Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hesabia asubuhi yako

Tuanze mwanzo kabisa– mission yako ni kutaka kulala vizuri na kuamka vizuri bila ya kuconfuse mwili wako. Ni vizuri kama utaamka muda huohuo kila siku ili kupanga kulala kwako na kuamka kwako. Kama utahitaji kuongeza au kuboresha zaidi jiulize maswali machache kuhusu siku nzima hapo ndio italeta tofauti

Usitumie kahawa mapema unapoamka. Tumia maji ya limau yenye uvuguvugu, halafu ikifika saa nne pata breakfast ya nguvu yenye proteins ya kusha pamoja na carbohydrates kiasi .
 
Chakula cha jioni

Kwenda kulala iwe ni muda ule ule kila siku. Epuka vyakula vya mafuta mengi, kula kiasi , epuka vinywaji vyenye kileo, kwa kuwa vitaharibu mpangilio wako wa kulala. Fanya meditation kabla ya kwenda kulala, itakusaidia kuwa na usingizi bora na kuuandaa mwili wako vizuri. Lala kwenye chumba cha utulivu.
 
Mbinu za kukusaidia uweze kulala vizuri usiku.

Kama una tatizo la wasiwasi, au woga, ni vizuri kama utaanza kutuliza akili yako kwa meditation kabla ya kulala usiku. Angalia na position unayotumia wakati unalala, Ni vizuri kama utaweza kulalia mkono wako wa kushoto kwa faida ya moyo wako, mgongo na mfumo mzuri wa tumbo lako.
 
Halafu fikiria kitu cha kuvaa wakati wa kulala. Mimi nakushauri ulale bila nguo. Lakini jifunike nguo nzito , kama blanketi sehemu za baridi . Kwa sababu wachunguzi waliona hilo kuwa kulala uchi itakusaidia kuepuka magonjwa ya ngozi na kupunguza hatari ya kupata kisukari aina ya pili. Na zaidi itarahisisha maisha. Hutakuwa na nguo nyingi za kufua kila mara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…