Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unaweza kubadilisha ubongo wako kwa kuwa mtu wa shukurani, na iwe ndio tabia yako ya kila siku. Andika kwenye notebook yako vitu ambavyo unashukuru.

Inaweza kuwa kwa ajili ya chakula cha pamoja , au hata wakati wa kwenda kulala na wakati wa kuamka.Utaona faida zake baada ya muda mfupi .
 
2.Zoezi la kuishi wakati uliopo

Huwezi kuwa mwenye nguvu kama utakuwa unakumbuka mambo mabaya yaliopita au kufikiria mambo mabaya ambayo yatatokea baadae. Ishi Wakati Uliopo. Na ndio wakati pekee ambao utaweza kubadilisha tabia yako.Ni muhimu sana kufocus muda ulipo sasa.kwa sababu kesho bado haijafika na jana imepita.
 
Ukifanya hivyo utapunguza stress na kupata faida nyingi kwa ajili ya afya yako.kwa hio pata dakika za kulenga kitu ambacho kimekuzunguka wakati huo. Sikiliza na uone kitu gani kinakupa amani.Tazama mahali ulipo unatambua kitu gani. Unahisi kitu gani.

Kwa kufanya hivyo utagundua kitu ambacho ni kigumu cha kufanya wakati huo, na utaanza kufurahia wakati uliopo kwa sababu hutakuwa na stress za matatizo ya jana wala yanayokuja.
 
3.Act ‘’as if.’’

Inaweza ikawa kama jaribu kubwa kusubiri mpaka uanze kuona mabadiliko. Lakini kusubiri mpaka uanze kujisikia vizuri kuhusu mwenyewe unaweza kuona kama moto unawaka.

Wachunguzi wanaamini kwamba ni bora kuishi na kutenda kama vile mtu ambaye unataka uwe badala ya kusubiri uone matokeo. Hapo ndio hisia zako na tabia zako zitafuata .

Unapojisikia kuwa na huzuni, badilisha huzuni kwa furaha , tafuta kitu ambacho kitakufanya uwe mwenye furaha.boresha hali yako.
 
Usitegemee ujasiri uje kutoka kusipofahamika. Badala yake jiulize, nitafanyaje kwa ujasiri? Halafu fanya kama mtu mwenye ujasiri. Hata kama unajihisi kuwa na mashaka. Saidia hisia zako ziwe kweli. Kujifanya kuwa mwenye ujasiri utawavutia watu wenye ujasiri kuja kwako.

Jaribu kujiuliza , watu wenye akili za nguvu wanafanyaje? Halafu fanya kama unajisikia mwenye nguvu tayari. Na utakua kwa jinsi hio.
 
Fanya push up kila siku kwa ajili ya kujenga akili yenye nguvu, zoezi rahisi na fupi , kama ukifanya kwa ziada zaidi utaweza kupata matokeo haraka.

Uwe makini na tabia ambazo zinaiba hisia zako nzuri na kuleta hisia mbaya. Kuanza kukata tamaa ya maisha kwa sababu ya kushindwa. Achana na tabia mbaya , itakusaidia kuwa smart, hakuna ugumu.

Kila la heri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…