Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MANCHESTER United imeamua kuachana na uhamisho wa kumchukua mlinzi wa Leicester City na timu ya taifa ya England, Harry Maguire na sasa imeelekeza nguvu zao zote katika kumnasa mlinzi wa Barcelona na timu ya taifa ya Colombia, Yerry Mina.
 
Mtaalamu wa masuala ya uhamisho wa wachezaji Manchester United, Matt Judge amesafiri mpaka Hispania kuanza mazungumzo na klabu hiyo ya Catalunya kwa ajili ya kumnasa Mina ambaye Barcelona wapo tayari kumuuza licha ya kuwasili klabuni hapo Januari mwaka huu.
 
Awali chaguo la kwanza la United lilikuwa Maguire lakini mabosi wa timu hiyo wamegundua kwamba staa huyo aliyetamba katika michuano ya kombe la dunia atapatikana kwa dau ghali la pauni 65 milioni na wameamua kumchukua Mina ambaye atapatikana kwa dau la chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…