FOUNDATION PROGRAMME
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinapenda kukujuza juu ya maswali na majibu kadhaa kuhusiana na Programme ya Foundation. Karibu tukujuze.
1. Foundation Programme ni nini?
Foundation Programme ni Programme ya maandalizi ambayo inawawezesha wanafunzi waliopungukiwa sifa kidogo za kujiunga na degree ya kwanza kuongeza sifa na mara baada ya kufaulu ndipo sasa wanaweza kujiunga na degree. Wanafunzi waliopungukiwa sifa ni wale waliohitimu kidato cha sita na Diploma.
2. Foundation Programme Imepewa Ithibati?
Foundation Programme ya Chuo Kikuu Huria pekee ndiyo ambayo imepata ithibati. Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imeruhusu Foundation Programme ya Chuo Kikuu Huria kuanza kufundishwa katika mwaka huu wa masomo wa 2018/2019 baada ya mtaala wake kutimiza vigezo vyote vya ubora na viwango.
3. Mwanafunzi akihitimu Foundation Programme anaweza kujiunga na Degree chuo kikuu chochote?
Mhitimu wa Foundation Programme ambaye atafaulu kwa viwango vilivyowekwa atakuwa amepata sifa za kujiunga na degree katika chuo chochote hapa nchini. Mhitimu huyo atashindana na wahitimu wengine katika kuomba degree na akishinda katika ushindani husika ataingia kwenye degree bila shaka yoyote.
4. Foundation Programme inatolewa na chuo gani?
Foundation Programme inatolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania pekee lakini mhitimu akimaliza anaweza kwenda kujiunga na degree chuo kingine. Hakuna chuo kikuu kingine kinachotoa foundation isipokuwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
5. Foundation Programme husomwa kwa Muda gani?
Foundation Programme ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania husomwa kwa mwaka mmoja wa Masomo na baada ya hapo ndipo anaweza kujiunga kusoma degree.
6. Ada ya Foundation Programme ni shillingi ngapi?
Ada ya Foundation Programme ni 635,000/= na inalipwa kwa awamu mbili. Mwanafunzi atalipa 320,000/= kwa awamu ya kwanza na 315,000/= awamu ya pili.
7. Foundation Programme ziliwahi kuzuiliwa?
Ndio TCU walizuia Foundation zote mwaka 2016 kutokana na baadhi ya Vyuo kuanzisha Foundation ambazo hazikuwa na ubora. Baada ya mapitio makini ya TCU imeridhika kuwa Mtaala wa Foundation Programme ndio uliweza kuwa na viwango vinavyotakiwa na kuruhusiwa. TCU wameruhusu baada ya kufanyiwa maboresho stahiki kwa mtaala husika.
8. Kwa nini Foundation ya Chuo Kikuu Huria pekee ndio iliyoruhusiwa?
Mtaala wake umekidhi viwango vyote. Pia ni jukumu la Chuo Kikuu Huria chochote duniani kutoa Programme za Foundation. Ndio maana Foundation Programme ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ilikuwepo tangu 1996. Wengine waliokuwa wameanzisha Foundation walichukua jukumu ambalo sio lao na hatimaye kuwa na Foundation zisizo na viwango.
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina matawi katika mikoa yote Tanzania bara na katika visiwa vya Unguja na Pemba. Pia kuna matawi katika baadhi ya wilaya. Hivyo ni rahisi kuwafikia Wananchi wengi kwa gharama nafuu kuliko taasisi nyingine yoyote ya elimu ya juu.
9. Sifa za kujiunga na Foundation Programme?
Sifa za kujiunga ni:
(a) Mhitimu wa kidato cha sita mwenye ufaulu wa wastani wa pointi 1.5 yaani angalau E na S kwenye masomo mawili.
(b) Mhitimu wa Diploma mwenye ufaulu wa GPA kuanzia 2.9 mpaka 2.0
(c) Mhitimu wa NTA level 5
Chuo Kikuu Huria kinawakaribisha wote wenye sifa tajwa walete maombi yao kabla ya tarehe 31/08/2018. Masomo yataanza rasmi mwezi Octoba 2018. Fomu za maombi zinatolewa bure katika matawi yetu yote nchi nzima. Huna haja ya kuja Dar es Salaam.
Maombi pia yanaweza kutumwa moja kwa moja kupitia tovuti ya chuo ambayo ni
www.out.ac.tz na kwa mawasiliano zaidi tupigie kupitia nambari 0719017254.
Mwisho, tunapenda kuwaalika wananchi wote wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya Mwanza, Mara na Shinyanga kutembelea banda letu katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika hapa Bariadi. Karibuni mtapata fursa ya kufanya maombi bure bila malipo.
Imetolewa na:
Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
03/08/2018
Bariadi Simiyu
Kwenye Maonesho ya Nanenane kitaifa.