Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Atletico Madrid
Diego Simeone tayari ameshaitegeneza Atletico Madrid kwa kuwanunua Thomas Lemar, Gelson Martins, Rodri na Santiago Arias, lakini anataka kuongezea nguvu kidogo.
Taarifa zinasema Luciano Vietto na Kevin Gameiro wote wanapewa nafasi ya kujiunga na miamba hiyo.
 
Manchester City
Mabingwa wa England wanaonekana wamemaliza usajili wao mapema, wakiwa wamezipata saini za Riyad Mahrez na Philippe Sandler.
Wamemaliza biashara yao, labda itoke nafasi ya kipekee au waondokewe na mchezaji na kulazimika kuziba pengo hilo.
 
Chelsea
Jorginho ametua ndani ya Stamford Bridge, na uhamisho unaozunguka katika klabu hiyo ni hatma ya Willian, Eden Hazard na Thibaut Courtois, ambao wanatajwa kuwa wanataka kuondoka, hivyo watatafuta wa kuziba nafasi hizo.
 
Manchester United
Jose Mourinho anataka kusajili nyota wa kuungana na Fred na Diogo Dalot katika kikosi cha Old Trafford msimu huu.
Kocha huyo amekuwa katika jitihada zake za kujenga kikosi chake, hivi karibuni amekuwa akihusishwa na kutaka kumsajili Yerry Minathe.
 
Juventus
Cristiano Ronaldo amejiunga na Juventus, lakini wamempoteza Gonzalo Higuain aliyejiunga na AC Milan hivyo watakuwa na upungufu wa wawashambuliaji.
Pia amepata pigo goli baada ya mkongwe Gianluigi Buffon kuondoka na kuiacha timu kwa Wojciech Szczcsny na Mattia Perin .
 
Paris Saint-Germain
Usajili mkubwa kwa PSG hadi sasa ni ule wa kuhakikisha Neymar haondoki.
Mabingwa hao wa Ufaransa, pia wanaweza kuwakosa Rabiot au Goncalo Guedes hivyo wanaweza kurudi sokoni kwa ajili ya kununua mchezaji wa kuziba pengo.
 
Bayern Munich
Imekuwa kimya katika uhamisho huu kwa Bavaria, huku Bayern Munich ikiwa imesajili nyota wawili tu akiwemo kiungo Leon Goretzka na kocha mpya Niko Kovac.
Hata hivyo, kuna uwezekano wa kuondoka kwa nyota wake Thiago au James .
 
Klabu za Ligi Kuu England zimetumia zaidi ya pauni 217milioni kulipa mishahara ya wachezaji majeruhi msimu 2017-18, kwa mujibu wa utafiti wa insurance broker JLT Specialty.
Gharama hizo zimeongezeka kwa asilimia 21% kutoka pauni176.6milioni ya msimu wa 2016-17, pamoja na kuwa idadi ya majeruhi imepungua kutoka 735 hadi 663.
 
Arsenal inaongoza kwa kuwa idadi ya majeruhi 54 msimu uliopita katika Ligi Kuu England.
Majeruhi ya misuri ndiyo yaliyowapata wachezaji wengi, wakati majeruhi ya goti yameongoza kwa kulipiwa fedha nyingi zaidi ikiwa ni wastani wa pauni 613,402 kwa mgonjwa.
Mabingwa Manchester City inashika nafasi ya pili kwa kuwa na majeruhi wachache msimu uliopita 24 tu, sawa na Newcastle, huku Brighton ikiwa na majeruhi wachache zaidi (15) ikiwa imelipa (pauni 3.01milioni) kwa wachezaji majeruhi.
JLT Specialty ilipiga hesabu kwa majeruhi hao kughalimu klabu kiasi cha mshahara wa pauni323,000.
 
Msimamo wa majeruhi kwa klabu 2017/18
Klabu Gharama (£m*) Idadi ya majeruhi
Manchester United 23.3 37
Arsenal 19.3 54
Liverpool 16.2 44
Chelsea 16 38
Everton 15.9 35
Crystal Palace 15.8 35
West Ham 14.8 50
Manchester City 13.9 24
Watford 11 37
Tottenham 10.5 33
West Brom 8 34
Swansea 7.3 27
Burnley 7 26
Stoke 6.5 30
Leicester 6 30
Bournemouth 5.7 35
Southampton 5.1 25
Newcastle 4.5 24
Huddersfield 4 30
Brighton 3 15
 
Mlinzi mahiri Leonardo Bonucci amerejea Juventus akitokea AC Milan huku akipishana na Gonzalo Higuain ambaye ametoka Juventus na kutua AC Milan.
Bonucci aliichezea kwa mafanikio makubwa Juventus akitwaa mataji sita ya Ligi Kuu Italia ‘Serie A’ kabla ya kwenda Milan
Wakati mlinzi huyo wa kimataifa wa Italia, akirejea Juventus mshambuliaji Gonzalo Higuain yeye ameuzwa kwa mkopo kutoka Juventus, kwenda Milan, ambayo italazimika kulipa Pauni 16 milioni lakini itaweza kumnunua jumla iwapo italipa Pauni 36 milioni.
Pia mlinzi Mattia Caldara mwenye miaka 24 naye ameamua kwenda kusaka maisha mapya AC Milan akitokea Juventus.
Higuain, alikua akihusishwa sana kutua Chelsea, baada ya Ronaldo kutua Juventus, lakini tofauti na matarajio ya wengi ameamua kwenda AC Milan.
 
MABOSI wa Manchester United wamekaa chini, wakatafakari, wakaona kuna umuhimu wa kumpiga faini staa wao, Anthony Martial, 22, aliyeondoka kambi ya timu yao pale Marekani na kurudi Ufaransa kushuhudia mpenzi wake akijifungua lakini baada ya hapo akagoma kurudi Marekani.

Hata hivyo, staa huyo ametunisha kifua na kudai hajali sana suala hilo kwa vile kwake yeye familia ni kitu cha kwanza kabisa kuliko Manchester United. Na sasa hali ya baadaye ya staa huyo imekaa hewani tu.
 
Juzi Martial alithibitisha anarudi katika mazoezi ya Manchester United ikiwa ni wiki moja tangu atoweke katika kambi hiyo Los Angeles huku Kocha Jose Mourinho akitazamia labda staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa angerejea Marekani.

Mourinho alimtaka Martial arejee Marekani baada ya kushuhudia mpenzi wake, Melanie Da Cruz kujifungua moto wa kiume aliyeitwa Swan. Hata hivyo, hadi wakati United ikicheza mechi ya mwisho ya kirafiki dhidi ya Real Madrid na kushinda 2-1 bado Mourinho alikuwa hajui kama Martial ataungana na wenzake wiki hii.
 
Hata hivyo, juzi Martial alituma ujumbe kupitia mtandao wake wa Twitter akiwashukuru mashabiki waliompongeza kwa kupata mtoto huku akisisitiza familia yake ni kitu cha kwanza kuliko kitu kingine chochote.

“Asanteni wote kwa salamu zenu. Mtoto wangu mchanga,Swan anaendelea poa, kwa mama mtoto mambo yalikuwa magumu lakini namshukuru Mungu anaendelea vema sasa. Samahani lakini familia yangu inakuja kwanza kuliko kitu chochote. Kesho Alhamisi (jana) narudi Manchester,” alisema Martial.
 
Na sasa uhusiano kati ya staa huyo na Mourinho umekaribia kutoweka kabisa na inadaiwa Mourinho anataka kumuuza kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Agosti 9 ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England.

Awali, Martial ambaye alitua Old Trafford miaka mitatu iliyopita akitokea Monaco kwa dau la Pauni 36 milioni aliwaambia marafiki zake asingerudi tena katika kambi ya United iliyowekwa Hoteli ya The Montage eneo la Beverly Hills ikiwa ni kujaribu kutimiza lengo lake la kutaka kuondoka Old Trafford.
 
Baada ya kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Liverpool jijini Michigan Jumamosi, Mourinho alimtaka Martial arudi huku akisema: “Ana mtoto na baada ya mtoto kuzaliwa, mtoto mrembo, aliyejaa afya njema, asante Mungu, alitakiwa arudi hapa na sio kuwa kule,” alisema Mourinho.

Tayari Mourinho kuna uwezekano akaanza ligi bila ya kuwa na wachezaji wengi mahiri ambao likizo zao ziliongezwa kutokana na timu zao kufika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kule Russia.

Hata hivyo, habari njema kwake ni kitendo cha mshambuliaji wake wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku kuamua kukatisha ziara yake na kujiunga na kambi ya timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mwanzo wa msimu mpya.
 
Wengine ni mastaa wawili wa England, Marcus Rashford na Phil Jones ambao wamekatisha ziara zao kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanaweza kupatikana kwa pambano la kwanza dhidi ya Leicester City Ijumaa ijayo.

“Tutaanza Ligi Kuu ndani ya siku nane na wachezaji hawa akiwemo pia na Victor Lindelof, aliyeanza mazoezi siku mbili zilizopita, Marcus Rashford, Jones na Lukaku wataanza kwa sababu wamekatisha likizo zao kwa siku tatu,” alisema Mourinho.

“Wanarudi siku tatu mapema zaidi kwa ajili ya kujaribu kucheza katika mechi ya kwanza. Na kwa ari ambayo tunayo kwa wachezaji wengi, narudia, kwa wachezaji wengi, basi tuna kila sababu ya kuanza LIgi Kuu vema,” alisema kocha huyo.
 

Attachments

  • Screenshot_20180803-194111~2.jpg
    Screenshot_20180803-194111~2.jpg
    79.5 KB · Views: 28
Back
Top Bottom