Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mpiga Picha; Mwalimu Mkuu Nitakuchaji Kila Mwanafunzi Sh. 500 Kwa Ajili Ya Pasport Size.

Mwalimu Mkuu: Mwalimu Waambie Wanafunzi Walete Sh, 1000 Kila Mmoja Kwa Ajili Ya Pasport Size.

Mwalimu: Wanafunzi Mnatakiwa Mlete Sh 2000 Kila Mmoja Kwa Ajili Ya Paspot Size.

Kila Mwanafunzi Nyumbani Kwao: Mama Tumeambiwa Tupeleke Sh 2500 Shuleni Kwa Ajili Ya Pasport Size.

Mama: Mme Wangu Mtoto Anataka Sh 3000 Kwa Ajili Ya Zile Picha Za Pasport Size Shuleni.

Unadhani Kwa Style Hiyo Ufisadi Utaisha??

Muwe Na Siku Njema.
 
Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri, anaonekana kuweweseka kutokana na kipigo cha mabao 2-0 ilichokipata kutoka kwa Manchester City katika mchezo wa Ngao ya Jamii hapo jana.

Sarri alisema kuwa kipigo hicho kimetokana na kuwakosa wachezaji wake sita wa kikosi cha kwanza, kauli iliyoungwa mkono na mchambuzi wa soka na mwanahabari Paolo Bandini.
 
Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja. Kuna:-
1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/
wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita "vishohia".
2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu.
3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchinja... wengi wanamiliki mabucha. Wana hasira sana na ni wakatili.. Akikuchoma kisu, siku ya mazishi anakuja kudai kisu chake.
4. WAMACHAME; hawa ni wezi sana, ukifanya nae dili umeliwa. Ni wasiri sana lakini wako makini mno hasa kwenye pesa. Wakiwa na hasira hawaoneshi waziwazi, so Mmachame anaweza kukuua huku akitabasamu. Sio waaminifu sana lakini wanaenda kanisani mara nyingi zaidi kuliko Wachaga wote. Wanawake wa machame wanaitwa 'Wapalestina'.. Mume ukitajirika mkeo anakuua ili arithi mali.
5. WAURU; hawa hupenda kusoma sana lakini hawapendi maendeleo kabisa. Hadi leo eneo lao la Kishumundu linatumika ku-identify wachagga washamba. Wanawake wakifikisha umri wa miaka 40 hua wehu na wanaume huwa vichaa mapema zaidi. Wanaume ni wavivu, lakini wanawake ni wachapakazi hodari. Wanazurura mjini na mabeseni wakiuza ndizi mbivu.. Ukioa Uru jiandae kulea kichaa.
6. WASIHA; Kwanza hawapendi kuitwa Wachagga. Wanajiita watu wa West-Kilimanjar
o. Ni mchanganyiko wa Wachagga na WaMeru. Hawapendi shule ila wanapenda zaidi kazi za ufundi na kilimo. Viazi vingi vya Chips Arusha na Moshi vinatoka kwao. Wanawake zao wana "vigimbi" mguuni sababu ya kulima mno.!
7. WAKIRUA; wanapenda sifa kama Wahaya. Wanawake wa Kirua ni wachawi kupindukia.. Wanaloga hata jiwe ili tu alikomoe.. Wanaume wa Kirua hawapendi kuoa kwao.. Hawapendi kuishi mjini maana wanaogopa gharama.. lakini siku wakija mjini wawili tu utadhani wako mia.
8. WA OLD-MOSHI; Hawa ni mafundi stadi wa ujenzi wa nyumba, japo hawajengi kwao. Mpaka leo hamna daladala ya kwenda Old-Moshi inayoanzia Moshi mjini, maana ni wabishi kulipa nauli na pesa inaishia kwenye mbege njiani. Wanaume wamezoea kutoka nyumbani saa kumi na moja alfajiri na kurudi saa sita ya usiku kwa miguu.!
 
Akizungumzia kipigo hicho Bandini alisema Chelsea ilizidiwa kutokana na kukosekana kwa wachezaji muhimu na akaenda mbali kwa kusema anamuunga mkono Sarri kupinga Eden Hazard na Thibaut Courtois wosiuzwe kwenda Real Madrid, kama timu hiyo inataka mafanikio msimu huu.
 
Nadhani hatupaswi kumlaumu wala kumbeza Sarri kwa Chelsea kufungwa 2-0 na Manchester City iliyokamilika, kuwakosa wachezaji sita muhimu kwenye timu ni pengo kubwa,” alisema.

Kati ya wachezaji walioshiriki fainali za Kombe la Dunia Russia, Juni na Julai mwaka huu, Chelsea iliwatumia wachezaji watano pekee ambao ni Willian, Antonio Rudiger, Cesar Azpilicueta, Victor Moses na Wily Caballero, katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Wembley.
 
Wachezaji muhimu ambao Chelsea iliwakosa ni pamoja na N'Golo Kante na Olivier Giroud wa Ufaransa, Thibaut Courtois na Eden Hazard wa Ubelgiji, pamoja na Waingereza nahodha Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek.

Kutokana na wachezaji hao sita kutoripoti hadi jana ni wazi kuwa Chelsea itawakosa pia katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England, wikiendi ijayo watakayoanzia ugenini dhidi ya Huddersfield, pengine yakawakuta yale ya msimu uliopita ya kuanza vibaya.
 
Mbali ya kuwakosa nyota hao Sarri pia alijitetea kwa ugeni akisema wachezaji wake bado hawajauelewa mfumo wake kwani ndio kwanza yupo katika wiki ya tatu tangu aanze kazi ndani ya Chelsea.

“Sio kwamba najitetea kwa kusema haya, lakini ikumbukwe mimi ndiyo nina wiki ya tatu tangu nijiunge na Chelsea, wachezaji bado hawajauzoea mfumo wangu na pengine hata mimi bado sijajua namna nzuri zaidi ya kuwatumia wachezaji wangu,” alisema Sarri.
 
Hili dili lipo na linavutia kweli kweli. Manchester United ina mpango wa kuipa ofa Chelsea wabadilishane mastaa wao, Anthony Martial aende Stamford Bridge na Willian atue Old Trafford. Kuna uwekano dili hilo likafanyika kabla ya Ijumaa.

Wote wawili hawana uhusiano mzuri na klabu zao kwa sasa huku wakiwa wanatamani kuhama. Martial amekuwa hana uhusiano mzuri na kocha wake, Jose Mourinho baada ya kutokomea kusikojulikana mara baada ya kwenda Ufaransa kushuhudia kuzaliwa kwa mtoto wake wa pili wa kiume.
 
Staa huyo alipigwa faini ya pauni 180,000 na United baada ya kushindwa kurudi tena nchini Marekani kuungana na wenzake mara baada ya kupata ruhusa ya kwenda Paris kushuhudia mpenzi wake akijifungua mtoto wa kiume.

Inasemakana aliwaambia wenzake kwamba hana mpango wa kurudi tena Marekani kitu ambacho kilimkasirisha Mourinho ambaye anataka kuachana na staa huyo huku akipata faida ya kumpata Willian kutoka Chelsea bila ya pesa yoyote kutumika.
 
Kwa muda mrefu Mourinho amekuwa akimsaka Willian ambaye alikuwa mchezaji staa zaidi katika msimu aliotimuliwa Chelsea baada ya timu hiyo kufanya vibaya na Willian yuko tayari kufanya kazi tena na kocha huyo Mreno.

Tayari WIllian naye amekuwa na majanga yake katika kikosi cha Chelsea chini ya kocha mpya, Maurizio Sarri ambaye alikerwa na kitendo cha nyota huyo kuchelewa kujiunga na kambi yake kwa madai ya tatizo la hati yake ya kusafiria.
 
Kocha Sarri ambaye amejiunga klabuni hapo akitokea Lazio ya Italia amekiri kutofurahishwa na kitendo cha nyota huyo wa kimataifa wa Brazil huku akidai kwamba anataka kufanya maongezi naye kuhusu tukio hilo na mustakabali wake kwa ujumla.

“Nataka kuongea naye. Sina furaha na hali ilivyo lakini kabla sijajibu chochote nataka kuongea naye.” Alisema kocha huyo ambaye jana kikosi chake kilitazamiwa kucheza mechi ya ufunguzi wa msimu na Manchester City.
 
Wachezaji wote wanathaminishwa dau la pauni 75 milioni lakini Martial anaonekana kuwa na thamani zaidi kwa vile ni mdogo kwa Willian kwa miaka saba na kuna uwezekano United wakadai chochote kutokana na tofauti hiyo.

Katika dirisha hili Willian alikaribia kujiunga na Barcelona lakini klabu hiyo ya Catalunya ikachemsha kutokana na dau kubwa ambalo Chelsea walikuwa wanalitaka. Badala yake waliamua kumchukua winga mahiri wa Kibrazil, Malcom kutoka Bordeaux ya Ufaransa.
 
Upande wa Martial, yeye kupitia kwa wakala wake alishatangaza kutaka kuondoka Manchester United katika siku za mwanzo za ufunguzi wa dirisha hili lakini United walipania kumbakisha kuhofia kufanya kosa kama ambalo Mourinho alilifanya wakati akiwaruhusu Kevin de Bruyne na Mohamed Salah waondoke Chelsea.
 
Juventus na Bayern Munich pia zimekuwa zikimsaka staa huyo ambaye kutokana na kucheza dakika chache msimu uliopita alishindwa kupata nafasi ya kuwemo katika kikosi cha kocha Didier Deschamps cha Ufaransa ambacho kilitwaa taji la kombe la dunia nchini Russia mwezi uliopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…