Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya kusoma maelezo hayo niliandika, “…vitaarifa vya aina hii havipaswi kusambazwa mpaka viwe vimethibitishwa. Anayeleta taarifa anasema amechota kwingine na kuingiza humu, hana uhakika. Wanaotajwa ni watoto wa umri mdogo ambao kisheria hawapaswi kuanikwa. Mwishoni nikaomba kuwepo hadhari.

Hoja iliyoletwa kutetea usambazaji taarifa hiyo (na siyo habari) ni kwamba, “tayari imesambaa sana na inasaidia watu kukaa macho…” Nililazimika kufungua darasa.
 
Kusambaa kwa uzushi au madai hakufanyi yawe ya kweli au sahihi. Hakuna jina la mtu yeyote linalotajwa. Hakuna aliyepima chakula na kugundua kuna sumu. Hakuna anayejua kama kilicho katika chupa ni sumu; ni sumu gani; na nani anajua, kama kweli ni sumu, kuwa ni hiyohiyo iliyowekwa kwenye chakula kinachodaiwa kuwa na sumu.

Nani anajua kingetokea kwa wazazi wa mtoto mtuhumiwa? Kipimo cha hasira ni kipi? Je, kama yanayodaiwa siyo kweli, nani ashitakiwe pamoja na wazushi-watuhumiwa?
 
Taarifa hiyo haina jina la mwalimu yeyote wa shule. Hakuna mamlaka ya shule inayotajwa.

Hakuna majina ya watoto isipokuwa nyuso kwenye picha.

Hakuna jina la aliyehoji mtuhumiwa au “dada” anayedaiwa kutoa sumu. Hata madai yangekuwa kweli, mashauri ya wenye umri huo hufanyiwa chemba.

Mangapi ya aina hii yameonekana mitandaoni na kwenye makundi yetu? Yote ni ya waandishi; hata kama yako magazetini au yanasikika redioni na kuonekana kwenye televisheni. Lakini siyo ya waandishi wa habari; na waandikaji wake hawastahili kuonewa wivu.
 
Nyota ya Kocha Pep Guardiola imezidi kung’ara wakati kocha huyo anapotimiza miaka kumi tangu ajitose kwenye ukocha baada ya jana kuiwezesha Manchester City kutwaa Ngao ya Jamii.

Guardiola ametimiza mataji 24 tangu alipotundika daluga na kugeukia ukocha, ingawa alianza kazi hiyo kwa vibaya kwa Barcelona kuchapwa na Numancia na kufuatiwa na sare dhidi ya Racing.
 
Kocha huyo amekuwa na mafanikio kwa kila Klabu anayoiongoza misimu minne aliyoinoa Barcelona alitwa mataji 14, matatu ya LaLiga, mawili ya Kombe la Ligi, matatu ya Spanish Super Cups, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya European Super Cups na mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia.

Katika misimu mitatu aliyoinoa Bayern Munich ya Ujerumani alitwaa mataji saba matatu ya Bundesliga, mawili ya Kombe la Ligi, moja la European Super Cup na moja la Klabu Bingwa ya Dunia.
 
Msimu yake miwili ndani ya Manchester City, amesghatwaa mataji matatu Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Ligi.

Ndani ya City taji pekee analolisaka ni lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya ambalo klabu hiyo haijawahi kulitwaa mara ya mwisho klabu hiyo kutwaa taji la Ulaya ni msimu wa mwaka 1969/70 walipotwaa Kombe la Washindi.
 
Mshambuliaji nyota wa Liverpool aliyetwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu England msimu uliopita Mohammed ‘Mo’ Salah raia wa Misri, anatarajiwa kupata ushindani mkubwa katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu msimu huu.
 
Mo Salah alimpiku Harry Kane wa Tottenham katika mechi za mwisho mwisho katika Ligi Kuu England hivyo kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 32 dhidi ya 30 ya Kane katika mechi 38 za Ligi hiyo yakiwa ni mabao mengi katika misimu ya hivi karibuni.
 
Mo Salah alimpiku Harry Kane wa Tottenham katika mechi za mwisho mwisho katika Ligi Kuu England hivyo kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 32 dhidi ya 30 ya Kane katika mechi 38 za Ligi hiyo yakiwa ni mabao mengi katika misimu ya hivi karibuni.
 
Sergio Aguero. Manchester City.

Mbali ya Kane pia atakabiliwa na ushindani kutoka Sergio Aguero, ambaye jana aliifungia Manchester City mabao yote ilipoichapa Chelsea kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Mshambuliaji huyo aliibuka mfungaji bora wa Ligi msimu wa 2014-15, alipofunga mabao 21.
 
Romelu Lukaku. Manchester United.

Mshambuliaji mahiri wa Manchester United, Romelu Lukaku amedhihirisha kuwa alistahili kupewa jezi namba 9, msimu uliopita alifunga mabao 16 na kasi ya ufungaji aliyoionyesha katika fainali za Kombe la Dunia inadhihirisha atakuwa moto wa kuotea mbali msimu huu.
 
Pierre-Emerick Aubameyang. Arsenal.

Mshambuliaji mahiri kutoka Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang aliyehamishia makali yake Arsenal, akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani Januari mwaka huu kwa ada ya Pauni 56 milioni, alifunga mabao kumi katika mechi 13 aliyoichezea Arsenal chini ya Arsene Wenger na anatarajiwa kumpa mwanzo mzuri Kocha mpya Unai Emery
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…