Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Midabuo ndani ya Ruaha
FB_IMG_1533536029252.jpg
 
Wiki iliyopita nilikuwa na majibizano na mmoja wa wanakikundi kwenye mtandao binafsi wa WhatsApp.

Huyu ni miongoni mwa Watanzania wenye hamu na shauku ya kupelekeana salamu na taarifa mbalimbali za maandishi kwa njia ya mitandao iliyo katika simu zao za mkononi.

Tuseme huyu ni miongoni mwa Watanzania wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 40 wenye laini za simu.
 
Wanaamkiana, wanasambaziana taarifa za matukio, wanakopeshana, wanadaiana, wanalipana, wanacheka, kununa na kulia pamoja na kujuta pamoja.

Ni kwa njia hii baadhi ya wenye simu za mkononi zenye mitandao mbalimbali wanajiita “waandishi wa habari.” Kwa kufanya hivyo wameibua shutuma kutoka kwa baadhi ya wenye vyeti vya uandishi wa habari ambao wamelalamika kuwa kazi yao “imevamiwa na wasiokuwa waandishi.”
 
Huu basi, siyo tu mkasa; ni msiba wa aina yake kuona anayeitwa mwandishi wa habari anaonea wivu wanaotaka kujifananisha na waandishi wa habari!

Anatamani wangenyang’anywa simu au wangekatwa midomo; hapana, wangekatwa ndimi. Nani bora sasa kati ya mvamizi mtuhumiwa na anayeitwa mwandishi wa habari mwenye vyeti anayeona wivu kwa asiye na vyeti kuandika chochote kile na kujiita mwandishi wa habari?
 
Wivu si hoja. Nitokako husema, “Atachuba talima ntano” – asiyeona wivu haendelei.

Lakini ukiona mtu ana wivu, tena kwa kitu dhaifu na dhalili au mtu ambaye hana cha kuiga kutoka kwake, ujue mwenye wivu ni sawa na anayeonewa wivu.

Hii ndio maana maandishi mengine ya aina iliyoko kwenye mitandao mkononi, tunayakuta pia katika magazeti, redio na televisheni.
 
Ni kwa kuwa viwango ni vilevile – aliyekufa leo na aliyevunda, wote ni wafu. Kwa msingi huu, kuna haja ya kugawana maarifa juu ya matumizi bora ya mitandao mkononi.

Sasa niweke hapa mfano halisi wa kile nilichokumbana nacho katika kikundi chetu.

Mmoja wa washirika aliweka wiki iliyopita maelezo kuwa katika shule moja ya msingi nchini (anaitaja jina na wilaya), mwanafunzi mmoja ameweka sumu katika chakula cha wenzake akiwa na shabaha ya “kuua wanaomsumbua shuleni.”
 
Maelezo yanasema sumu hiyo alipewa na “dada mmoja; lakini chakula kilikuwa hakijafikishwa kwa walengwa” ndipo ikagundulika kwamba mtoto mtuhumiwa amehojiwa, “amefukuzwa shule na hatua nyingine zinafuata.”

Zaidi ya hayo, mpashaji akaweka picha za watoto wawili akiwatambulisha bila kutaja majina lakini kwa kuandika: “huyu ndiye aliye okoa wenzake” na mwingine, “aliye kusudia kuua wenzake huyu.”
 
Akaweka sahani yenye kinachoonekana kama wali na kuandika juu yake, “Chakula kilichowekwa sumu.” Pembeni akaweka kiganja kilichobeba kichupa cheupe chenye mfuniko wa rangi ya bluu na kuandika, “hii ndiyo sumu iliyotumika;” halafu akajikosha kwa kuandika kuwa amechukua tu na kubandika (siyo kazi ya mikono yake)
 
Back
Top Bottom