MAJINA YA WAHAYA Mtoto wa kwanza anaweza kuitwa Kokubanza, kokutangilila, Lubanzibwa Kalimuna kama mtoto angezaliwa baada ya wazazi kukaa muda mrefu bila kupata mtoto, mtoto aliyezaliwa aliitwa ama Mushumbusi, Shumbusho, Rwezaula, kukulingilila, kokumalamala au Mkaanguki Kama baba angekufa akamwacha mke wake ana mimba, mtoto aliyezaliwa aliitwa Kabwanga wa kike, kasigwa au kashangaki wa kiume Pacha wa kiume aliyezaliwa kwanza aliitwa Ishengoma au Kakulu wa kike aliitwa Nyangoma, Pacha wapili kama ni wakiume aliitwa Kato. Wa kike alitwa Nyakato Mtoto aliyezaliwa akiwafuata mapacha wakiume aliitwa Kyaluzi wa kike aliitwa Mkabaluzi Kwa wahaya mapacha si tu watoto wanaozaliwa wawili, hata mtoto mmoja anayezaliwa kwa kutanguliza miguu huitwa pacha tena huyu ndiye huitwa pacha halisi. Kwa wahaya huita ‘eilongo alikulu’ Majina mengi ya kike huanza na KOKU mfano Kokushubila, kukoshobokelwa, Kokugonza nay a kiume huanza na Ruta kama Lutakulembelwa, Lutanywana, Lutasingwa Kuna matumizi ya herufi ya R na H katika lugha ya luhaya sijayaelewa vizuri maana katika kuongea kwa wahaya uwezi kusikia mtu anajiita muhaya utamsikia anajiita muaya, utasikia anajiita Lweyemamu sio Rweyemamu Wanawake wa Kihaya hutakiwa kulima heka za Maharagwe kwa ajili ya matumizi ya kaya yake na hawapaswi kusaidiwa na mumewe hata kama ni heka 10 MAJANGA YALIYO WAKUMBA WAHAYA Majanga yanayozungumziwa mara kwa mara ni vita ya Idd Amin, ugonjwa wa UKIMWI , kuzama kwa meli ya MV BUKOBA, anguko la bei ya kahawa na kwa sasa tetemeko la ardhi Ni matumaini yangu kwamba umejifunza kitu kupitia historia hii fup