Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Samahani mkuu, nilighafirika
Marhabaaaaaaa! Habari ya mwamko mkuu wangu..
 
Baada ya kuomba kuuzwa rasmi, Siku ya Jana Thibaut Courtois ameshindwa kuripoti mazoezini kama alivyotakiwa baada ya muda mapumziko kuisha. Inaripotiwa Courtois hajafika mazoezini ili kuonyesha msisitizo kwamba anataka kuondoka na ameonekan mjini Tenerife - Spain mchana wa leo wakati wenzake wote wakiwa mazoezini London.
 
KAMA unadhani mastaa wa Real Madrid wamefurahishwa na hatua ya mabosi zao kumuuza Cristiano Ronaldo, basi utakuwa unajidanganya sana na Toni Kroos ameamua kufunguka.

Kiungo huyo wa Kijerumani amefichua kuwa, kuondoka kwa Ronaldo kumeacha pengo kubwa na watapata sana kupata mtu wa kuziba nafasi yake hasa katika kupasia nyavuni.
 
Ronaldo, ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or mara tano, ameachana na Madrid na kutua zake Juventus kwa dau la Euro 112 milioni huku akiibeba Los Blancos kubeba mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kroos amesema, haitakuwa shida kuanza msimu mpya bila Ronaldo, lakini kwenye kupachika mabao itakuwa suala gumu kwani, Mreno huyo alikuwa fundi na data zake zimekuwa juu muda wote.
 
Mabao 50 kwa msimu sio kitu kidogo kabisa, Ronaldo ameifanya kazi yake vizuri na itakuwa vigumu sana kupata mtu wa kuifikia rekodi yake,” alisema Kroos.

“Cristiano alikuwa mtu muhimu katika timu kwa miaka kadhaa sasa, uwepo wake umetufanya bora uwanjani na kushinda mataji, lakini tutapata tabu sana hasa tukikutana na Juventus msimu huu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.”
 
JOSE Mourinho amewaziba midomo wachambuzi wa soka wanamponda kuwa hampi kinda wake, Marcus Rashford muda wa kutosha uwanjani ili kuonyesha na kukuza kiwango chake.

Lakini katika kuonyesha kuwa anawajali vijana, Mreno huyo ameamua kumkabidhi Rashford jezi namba 10 ambayo imekuwa ikitumiwa na mastaa wakubwa ndani ya kikosi hicho.
 
Awali, Rashford alikuwa akivaa jezi namba 19, lakini sasa amepewa namba 10 iliyokuwa ikitumiwa na mastaa kama Mark Hughes, Teddy Sheringham, Ruud van Nistelrooy, Wayne Rooney na mwisho alikuwa Zlatan Ibrahimovic.

Kwa mara ya kwanza, Rashford alivaa jezi hiyo kwenye mchezo wa kirafiki wa juzi Jumapili usiku dhidi ya Bayern Munich, ambapo ni mara ya pili kubadilishiwa jezi chini ya Mourinho.
 
Wakati akipandishwa kwenye kikosi cha wakubwa, kinda huyo alikuwa akivaa jezi namba 39.

Kwa kupewa jezi namba hiyo, ni wazi Rashford ameanza kuaminiwa kwani jezi hiyo ni moja kati ya namba za heshima kwenye kikosi cha United.

“Ni rasmi sasa, Marcus Rashford ndio mmiliki wa jezi namba 10 wa Manchester United,” mtandao wa United uliandika.
 
DAKIKA za majeruhi katika dirisha la uhamisho pale England. zimebakia saa 72 tu kabla ya dirisha hilo kufungwa na Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anapambana na rekodi ya uhamisho kwa mabeki, iliyowekwa na mlinzi wa Liverpool, Virgil Van Dijik Januari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…