Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mcheza tenisi nyota wa Marekani, Serena Williams, amefichua kilichosababisha ajitoe kwenye michuano ya Rogers Cup inayoendelea nchini Canada.
Nyota huyo mwenye miaka 36, ni bingwa wa mataji 23 ya Grand Slam kwa wanawake kwa wachezaji mmoja mmoja, alisema aliamua kujitoa baada ya shutuma kuhusu mwanae kuzidi.
 
Alisema baada ya kushutumiwa sana na ndugu na jamaa zake alikaa na kutafakari kisha akabaini kuna ukweli kwamba yeye yu mkosaji kwa kumuacha mwanae wa miezi 11 na kwenda kushiriki mashindano ya tenisi.
“Mwanangu alizaliwa Septemba 2017, mimi tangu Julai nilishaanza kumuacha kwa saa nyingi nikijiandaa kwa mashindano ya Wimbledon badaye nimekuja huku kweli najiona mkosaji kwa mwanangu,” alisema.
 
Serena alichapwa kwa seti mbili za 6-1, 6-0 na Mwingereza Johanna Konta katika mashindano ya Silicon Valley Classic, ikiwa mara ya kwanza kwake kushindwa katika raundi ya awali ya michuano yoyote ile tangu mwaka 1995 alipoanza kucheza tenisi ya kulipwa.
Siku mbili baadaye ndipo akatangaza kujitoa kwenye Rogers Cup, jana aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram kwamba anajiona mkosaji kwa kutoyapa kipaumbele malezi ya binti yake.
 
Mchezaji tenisi wa Uingereza, Katie Boulter ameng’olewa katika raundi ya kwanza ya mashindano ya Rogers Cup yanayoendelea mjini Montreal, Canada.

Katie mwenye miaka 22, alipoteza mchezo dhidi ya Lesia Tsurenko wa Ukraine na kuendeleza msimu mbaya ambapo mwaka huu aliaga mashindano ya Wimbledon katika raundi ya pili.
 
Katika mchezo wa juzi, Lesia mwenye miaka 29, alimshinda kirahisi kwa seti mbili za 6-4 6-2 akitumia dakika 85.

Katie aliingia uwanjani akiwa na matumaini ya kushinda ili kupanda viwango vya ubora wa tenisi duniani kwa kuingia katika 100 bora kwa mara ya kwanza katika historia yake.
 
Katika mchezo mwingine kigogo wa tenisi wa Marekani Venus Williams alishinda dhidi ya Caroline Dolehide seti 7-5 6-1 sawa na Karolina Pliskova aliyepata ushindi wa seti 6-4 6-4 alipovaana na Katerina Siniakova.

Venus mwenye miaka 38 anaonekana kurejea katika kiwango chake cha ubora wa tenisi akiwa na mataji saba ya Grand Slam, alipangiwa kucheza na mshindi wa mchezo kati ya Sorana Cristea na Monica Niculescu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], siku moja nitakualika uje ujionee mwenyewe kama huwa naingia ndani ama nakomea nje.[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Naomba hiyo mechi iwe kati yako na Mwakaleli. Na popcorn nitaziagiza kutoka Yuropu kabisa. Na miwani mipya. Ili nikuone vizuri prof ukiburutwa na fenesi...kutoka kona moja ya kitanda hadi nyingine...hakuna pa kukimbilia isipokuwa kupokea kipigo kitakatifu kama kilivyo...Halafu yaani naona taswira kabisa laivu...Uzi huu shwainii kabisa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️
 
[emoji57][emoji57][emoji41][emoji41]
tapatalk_1533666612553.jpeg
 
Naomba hiyo mechi iwe kati yako na Mwakaleli. Na popcorn nitaziagiza kutoka Yuropu kabisa. Na miwani mipya. Ili nikuone vizuri prof ukiburutwa na fenesi...kutoka kona moja ya kitanda hadi nyingine...hakuna pa kukimbilia isipokuwa kupokea kipigo kitakatifu kama kilivyo...Halafu yaani naona taswira kabisa laivu...Uzi huu shwainii kabisa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], niache mie
 
Back
Top Bottom