Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mshambuliaji wa Liverpool Firmino ametoa msaada wa Pound zenye thamani ya zaidi ya Milioni 192 za Kitanzania kwa familia moja nchini Brazil ili zikisaidie kuwatibu Watoto wawili wa familia hiyo wanaougua ugonjwa unaowafanya washindwe kutembea na kupumua vizuri.
 
Mabao yaliyofungwa na beki wa Tottenham, Jan Vertonghen na Dele Alli yalitosha kuwanyamazisha Newcastle United katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu msimu huu wa 2018/19.

Mchezo uliopigwa muda mfupi uliopita kwenye uwanja wa James' Park na wenyeji kuondoka vichwa chini wakishindwa kuamini matokeo hayo.

Tottenham, timu iliyoandika historia kwa kuwa ya kwanza kutosajili mchezaji katika dirisha la kiangazi tangu kuasisiwa kwa mfumo wa usajili wa kiangazi mwaka 2003, iliutawala mchezo kwa kiasi kikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…