Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

428928020_235636.jpg
 
Shirika la anga la Marekani Nasa limehairisha shughuli ya kutuma chombo cha Satelaiti karibu na jua kuliko hapo awali.
Chombo hicho kinachojulikana kama Parker Solar Probe kilitarajiwa kuzinduliwa eneo la Cape Canaveral, Florida leo Jumamosi lakini uchunguzi wa dakika za mwisho umesababisha safari hiyo kuhairishwa.
 
Roketi hiyo ya Delta itaipeleka satelaiti anga za mbali ili iweze kupita sayari ya Venus kwa kipindi cha wiki sita zijazo kabla iendelee na safari yake kwenda kwa Jua kwa muda wa wiki zingine sita.
Katika kipindi cha miaka saba Parker itazunguka mara 24 kwa Chua ikijaribu kusoma fisikia ya corona, eneo ambalo shughuli nyingi zinaoathiri dunia hutokea
 
Mwalimu mkuu wa shule nchini Burundi amekamatwa kwa kudanganya kuwa yeye ni mwanafunzi akiwa na lengo la kumfanyia mtihani mtu mwingine.
Polisi waliingia kwenye ukumbi wa mtihani ambapo Benjamin Manirambona alikuwa akifanya mtihani huo.
Hakufahamu kuwa polisi ambao walikuwa wamevalia nguo za raia walikuwa waemsubiri usiku kucha shuleni ili wamkamate.
Bila ya kuwepo mahala pa kutorokea mwalimu huyo mkuu wa taasisi ya Butere alikiri papo hapo.
 
Back
Top Bottom