Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pindi tutakapo jiridhisha kuwa soko limechangamka tutaweka bei elekezi kwa wauzaji hao ambayo watatakiwa kuifuata,” anasema Kaguo.

Lakini huenda tangazo la kufikia ukomo wa matumizi ya mkaa Juni Mosi 2017 kulichangia kwa kiasi kikubwa uingizwaji wa gesi ya kupikia nchini na kufanya watu wapunguze matumizi ya mkaa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos anasema moja ya changamoto iliyokuwa ikifanya watu wasibadili matumizi ya mkaa ni upatikanaji wa nishati mbadala ya kupikia kwa uhakika na gharama nafuu tofauti na ile waliyoizoea.
 
Kama ni gesi basi ipatikane karibu na nyumba zao na hivi karibuni tulifanya kampeni nyingi ikiwamo ya kutangaza kuzuia matumizi ya mkaa Juni 2017, jambo ambalo lilichangia watu wengi kutafuta mbadala wa nishati ya mkaa ili kuepuka kuathirika na hatua ngumu zinazoweza kuchukuliwa,” anasema Santos.

Endapo uingizwaji wa gesi utaongezeka, itakuwa ni ahueni kwa misitu kwa sababu kitu kilichokuwa kikiweka changamoto katika kupiga vita matumizi ya mkaa ni kukosekana kwa nishati mbadala ya uhakika.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, jumla ya tani milioni tano za mkaa huzalishwa nchini kila mwaka zinatokana na ukataji wa misitu.
 
Mkurugenzi wa Sekta binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye anasema ongezeko la uingizwaji wa gesi ni habari njema pia ni ishara ya kuwa matumizi ya nishati ambazo zinaharibu mazingira utaanza kupungua na watu watahamia katika nishati ambazo ni rafiki wa mazingira

“Hata uzalishaji viwandani sasa utaongezeka kwa sababu vitaweza kuhamia katika matumizi ya gesi kuendesha shughuli zake za kila siku.

“Japo hata sasa baadhi ya washiriki wetu wanadai hali ya biashara imeanza kutengemaa baada ya watu kulalamika sana na kuamua kuiga namna ya kuishi ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano,” anaongeza.
 
Lakini kama nchi ina gesi ya asili kiasi cha futi za ujazo trilioni 57 katika eneo la Songosongo ambayo inatosha kwa matumizi ya nchi nzima lakini mpaka sasa ni nyumba 30 pekee ndizo zilizoweza kuunganishwa katika mradi wa majaribio huku nyumba nyingine 150 zikitarajia kuunganishwa katika mkoa wa Dar es Salaam kwa mujibu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Kapulya Musomba aliwahi kunukuliwa na gazeti hili akisema ujenzi holela wa nyumba katika baadhi ya miji umekuwa ni chanzo cha ucheleweshaji usambazaji wa gesi ya asilia majumbani.
 
Kwa kulitambua hilo, Ni vyema sasa mipango miji watakapo kuwa wanahitaji kuandaa ramani wakatushirikisha na sisi ili tuweze kuweka ramani madhubuti itakayotupatia urahisi katika kupitisha mabomba yetu ili kuwafikia wakazi wa majumbani,” anasema Musomba.

“Jambo hili limekwamisha kwa kiasi kikubwa katika kufikia adhma tuliyokuwa tumejiwekea ya kuweza kusambaza gesi katika nyumba 30,000 ndani ya mwaka mmoja na badala yake mpaka sasa ni nyumba 70 ndiyo zimefikiwa,” alisema Musomba
 
Mwanariadha Volha Mazuronak wa Belarus, jana alitwaa medali ya dhahabu katika mbio za marathon za ubingwa wa Ulaya 2018, kwa wanawake licha ya kukumbwa na kadhia ya kutokwa na damu puani.

Mwanariadha huyo mwenye miaka, 29, aliwapita kidogo Clemence Calvin wa Ufaransa na Eva Vrabcova Nyvltova wa Jamhuri ya Czech.

Mazuronak alitwaa ushindi baada ya kutumia saa 2:26.22 na mwanariadha huyo hakukata tamaa hata kidogo licha ya kujikuta akitokwa na damu nyingi puani dakika za mwanzo.
 
Baada ya damu kuzidi kutoka mwanariadha huyo alipunguza kasi kwa mwendo wa karibu maili moja na alipomaliza mbio hizo alipongezwa sana na waratibu.

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Dunia katika mbio za Marathon, Paula Radcliffe, alimmwagia sifa sana Mazuronak, kwa kichendo cha kumaliza mbio hizo licha ya kutokwa na damu nyingi.

“Kwa hakika Volha Mazuronak anastahili pongezi sana sio kwa sababu ya ushindi alioupata bali kwa ustahimilivu aliouonyesha katika mbio hizo,” alisema Radcliffe.

Nyota namba moja kwa Uingereza, Tracy Barlow, alimaliza katika nafasi ya 15, wakati kwa wanaume, Koen Naert wa Ubelgiji alishinda kwa wanaume akiandika muda bora was aa 2: 9.51 na Tadesse Abraham muethiopia aliyechukua uraia wa Uswisi, alishika nafsi ya pili huku Yassine Rachik wa Italia akishika nafasi ya tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…