Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Gwiji wa soka wa klabu ya Arsenal, Ian Wright, amechukizwa na ubaguzi wa rangi aliofanyiwa winga wa Manchester City na England, Raheem Sterling.

Akizungumzia tukio hilo lililotokea baada ya Arsenal kuchapwa mabao 2-0 na City katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England, Ian Wright alisema ni jambo la kuhuzunisha kuona mashabiki wa klabu hiyo wamefikia hatua hiyo.
 
Sterling mwenye miaka 23, aliifungia City bao la kwanza na alionyeshwa vitendo vya kibaguzi, akishambulia kwa visingizio mbali mbali ikiwemo kubwa kwa tattoo aliyoichora mguuni ikionyesha picha ya bunduki aina ya ‘rifle’, lakini baadhi wanadhani mafanikio yake ikiwemo kitendo cha kumnunulia mama yake mzazi nyumba kinawaumiza mengi.

Aidha mashabiki hao wamekuwa wakimuandamana mchezaji huyo kwa kusema alicheza chini ya kiwango katika fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Russia.
 
“Ni watu wangapi unaowafahamu ambao wamekuwa wakimpinga Sterling na kumbagua kwa sababu ya rangi yake," alihoji Wright.

Alisema suala la kupinga ubaguzi wa rangi ni kampeni inayomtaka kila mwanasoka kusimama kidete kuipinga pale anapoona ikifanyika lakini katika kadhia ya Raheem hakuona mchezaji yeyote aliyesimama na kumpigania kwa ubaguzi aliofanyiwa.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Chris Sutton, alisema anadhani athari za matokeo ya fainali za Kombe la Dunia zimeendelea kuwaathiri mashabiki wa soka nchini Uingereza bila kujali nafasi waliyoipata England kwenye fainali hizo.
 
Beki wa Chelsea, Antonio Rudiger amemmwagia sifa kipa mpya wa timu hiyo Kepa Arrizabalaga, akisema alionyesha kiwango cha hali ya juu na kuthibitisha thamani ya kuwa kipa ghali duniani.

Mchezaji huyo aliyenunuliwa katika dirisha la usajii wa kiangazi akitokea Athletic Bilbao, alionyesha kiwango cha juu Jumamosi iliyopita katika mchezo ambao Chelsea iliishinda mabao 3-0 Huddersfield Town, katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England.
 
Kutokana na kiwango alichokionyesha, kimemfanya Rudiger kumpongeza Kocha Maurizio Sarri kwa kumsajili kipa huyo chipukizi wa Hispania.

Alisema amefurahishwa na kiwango cha Kepa na kwamba anamtabiria makubwa Stamford Bridge na kwamba Chelsea haitakuwa na pengo la Thibaut Courtois, aliyeuzwa kwenda Real Madrid katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili.
 
Baada ya kuanza Ligi Kuu England kwa kishindo ikiitandika kwa mabao 4-0, West Ham United, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amefunguka na kusema timu hiyo ni bora zaidi ya alivyodhani.
Akizungumzia mchezo huo na namna anavyoiona Ligi kwa ujumla, Klopp alisema kuwa amestaajabu ubora wa kikosi chake kwani hakutarajia kuiona katika kiwango bora kama hicho.
 
Alisema hazungumzi hivyo kwa sababu ya ushindi bali tathmini ya mchezo ndiyo iliyomstaajabisha, kutokana na timu hiyo kumiliki mpira kwa kiwango cha juu.
Katika mchezo huo, mabao ya Liverpool yaliwekwa kimiani na Mohammed Salah, dakika ya 19 na Sadio Mane dakika ya 45 na kwenda mapumziko wakiongoza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Liverpool walijipatia bao la tatu likifungwa na Mane tena na Daniel Sturridge akahitimisha karamu hiyo ya mabao zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika.
 
Kwa kweli nimestaajabishwa na kiwango chetu, sikutarajia kuwa timu Ipo katika kiwango bora namna hii, kila mchezaji alitimiza wajibu wake kwa kiwango cha juu,” alisema.
Alisema timu inapoanza Ligi kwa ushindi inakuwa na nafasi nzuri ya kufanya vizuri katika mechi nyingi zinazofuata kutokana na wachezaji kujiamini.
 
Liverpool ambayo ilianza Ligi ikiwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Anfield, wikiendi hii itasafiri kuifuata Crystal Palace, kabla ya kuikaribisha Brighton katika mzunguko wa tatu wa Ligi hiyo.
 
Kinyang’anyiro cha Ligi Kuu England, kimeanza tangu wikiendi iliyopita, timu zinazotabiriwa kumaliza ndani ya nne bora, mabingwa watetezi Manchester City, Liverpool, Tottenham na Manchester United zikianza kwa kishindo.
Tottenham iliyoziengua Chelsea na Arsenal katika ‘top four’ ikitamba kwa msimu wa tatu mfululizo licha ya kujadiliwa sana kutokana na kutosajili mchezaji yeyote katika dirisha la usajili wa kiangazi, lakini imethitisha kuwa haikuwa na sababu za kusajili kwani inacho kikosi bora baada ya kushinda ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United.
 
Ujio wa Kocha, Maurizio Sarri, unaweza kuwa suluhisho kwa Chelsea, kwani aliiwezesha kushinda mabao 3-0 dhidi ya timu ngeni katika Ligi hiyo, Huddersfield Town, lakini wikiendi hii ndipo atapaswa kuthibitisha kama anao ubavu wa kuchuana kuing’oa Tottenham ndani ya nne bora.
Sarri atathibitisha hilo, atakapoiongoza Chelsea kuikaribisha Arsenal kwenye Uwanja wa Stamfodge Bridge, iwapo itaondoka na ushindi wa kishindo kama ilioupata kwa Huddersfield ataanza kuwashawishi wengi kuipa nafasi ya kufanya vema msimu huu.
Arsenal jana Jumapili iliyopita ilicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani bila Arsene Wenger kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996, licha ya kuwa nyumbani kocha Emery Unai hakuweza kuiepusha na adhabu kutoka kwa mabingwa watetezi City na kufungwa mabao 2-0.
 
Kocha wa kuwa huyo wikiendi ijayo pia atakuwa katika wakati mgumu kwani atasafiri kuifuata Chelsea moja ya timu ambazo zinaonekana zina vikosi bora vinavyoweza kupigania ubingwa.
Kwa upande wake Kocha City, Pep Guardiola alitamba kuwa kikosi chake kitazidi kutoa dozi kwa kila timu itakayocheza nayo akidai timu hiyo inamarika siku hadi siku.
Guardiola alisema kuwa anaamini katika mechi ijayo sio Bernardo Silva na Raheem Sterling pekee walioifungia mabao hayo, watakafunga tena wikiendi ijayo bali wafungaji wataongezeka watakapoikaribisha Huddersfield Jumapili hii.
 
Nayo Manchester United chini ya Jose Mourinho imeanza vema Ligi baada ya kuichapa timu bingwa ya Ligi hiyo msimu wa 2015/16, Leicester City kwa mabao 2-1 na wikiendi hii itaifuata timu isiyo na uzoefu ya Brighton.
Upande mwingine, Henrikh Mkhitaryan aliyehamia Arsenal akitokea United pamoja na washambuliaji mahiri Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette hawakuibeba Arsenal kama walivyofanya katika timu zao za zamani Aubameyang alikua tegemeo la mabao kwa Borussia Dortmund ya Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ na Lyon ya Ufaransa ‘Ligue 1’.
City ambayo iliilaza Chelsea mabao 2-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii inaonekana kuzidi kuimarika kila kukicha na sasa ni wazi kuwa inaweza kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji la Ligi Kuu.
 
City iliyomnunua Riyad Mahrez pekee katika dirisha la usajili wa kiangazi kwa Pauni 60 milioni kutoka Leicester City, alionyesha ana kitu amekiongeza kwa City.
Mitambo ya Liverpool inaonekana imeongezeka nguvu na imeonyesha dalili kuwa itaangamiza zaidi msimu huu baada ya Sadio Mane kufunga mawili, Mohamed Salah na Daniel Sturridge nao wakitupia, huku James Milner na Robeto Firmino, wakicheza soka la kiwango cha juu, hata hivyo Liverpool wikendi hii itakuwa ugenini ikiifuata Crystal Palace.
 
Back
Top Bottom