Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bobi Wine pia aliandika kuwa hoteli yake ilizingirwa na polisi kufuatia visa hivyo.
Hata hivyo polisi wanasema kuwa wafuasi wa upinzani watalaumiwa kwa kuuliwa dereva huyo wa Bobi Wine Yasin Kawuma.
Msemaji wa polisi Emilian Kayima, anasema watu waliokuwa wamevaa shati za kampeni za mgombea Wadri, walianza kuurushia mawe msafara wa rais hali ambayo ilisababisha polisi kufyatua risasi.
"Mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni msafara wa rais ulishambuliwa na wahuni katika manispaa ya Arua wakati rais alikuwa anaondoka uwanja wa Boma ambapo alikuwa amefanya mkutano wa mwisho," Kayima alisema.
 
Daraja la barabara ya mwendo kasi limevunjika huko kaskazini mwa Italia katika mji wa Genoa na kusababisha vifo vya watu wapatao 35.
Picha ya video inaonyesha upande mmoja wa mnara ulisababisha daraja kuanguka kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.
Takriban magari 30 yalianguka katika upande wa mfereji wa uchafu.
 
Waziri wa usafirishaji Danilo Toninelli ameliongelea janga hilo kuwa kubwa na Ufaransa nayo imehaidi kushirikiana pamoja na Italia katika janga hilo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameandika ujumbe wa pole katika ukurasa wake wa Twitter kwa waitaliano na wafaransa pia.
 
Majira ya saa tano na nusu (09:30 GMT) wakati wa mvua kubwa ,
''Polisi iliripoti juu ya mvua kubwa iliyokuwa inanyesha muda huohuo ndio nilipoona mwanga ukimulika katika daraja na mara daraja likaanza kushuka chini",shahidi alieleza
Shahidi mwingine alisema kwamba tulisikia muungurumo mkubwa na mwanzoni tulidhani kuwa ni radi ambayo iko karibu nao.
Naibu waziri wa usafirishaji wa nchi hiyo ,Edoardo Rixi amesema idadi ya vifo ni 35 lakini wanatarajia kuwa vifo hivyo vinaweza kuongezeka.
 
Majira ya saa tano na nusu (09:30 GMT) wakati wa mvua kubwa ,
''Polisi iliripoti juu ya mvua kubwa iliyokuwa inanyesha muda huohuo ndio nilipoona mwanga ukimulika katika daraja na mara daraja likaanza kushuka chini",shahidi alieleza
Shahidi mwingine alisema kwamba tulisikia muungurumo mkubwa na mwanzoni tulidhani kuwa ni radi ambayo iko karibu nao.
Naibu waziri wa usafirishaji wa nchi hiyo ,Edoardo Rixi amesema idadi ya vifo ni 35 lakini wanatarajia kuwa vifo hivyo vinaweza kuongezeka.
 
Daraja hilo ambalo lilijengwa tangu mwaka 1960,lilikuwa linawahudumia waitaliano na wafaransa ni miongoni mwa madaraja kumi nchini humo.
Serikali ya Italia hivi karibuni ilihaidi kuongeza kiwango cha uwekezaji katika miundombinu .
Mwaka 2006 taifa hilo lilitumia zaidi ya yuro bilioni 14 kwa ajili ya matengenezo ya barabara lakini mwaka 2010 kiasi hicho cha fedha kilipungua yuro bilioni nne kwa mujibu wa shirikisho la uchumi na maendeleo ( Economic Co-operation and Development).
 
Mwanamuziki na 'video vixen', Gigy Money amesema kuwa anatamani mtoto wake aje kuwa na tabia kama zake, kwa kuwa yeye anatengeneza pesa nyingi kutokana na maisha anayoishi.
 
Kitendo cha kukumbatiana sio tu kinaleta upendo na kuileta jamii pamoja bali kina faida kubwa za kiafya na kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa, watu hushauriwa kukumbatiana angalau mara 8 kwa siku.
Nimekusogezea hapa faida 10 za kukumbatiana.
 
Kumkumbatia mtu unayemjali au kumpenda kunasaidia ubongo kuzalisha homoni inayojulikana kama OXYTOCIN ambayo huusaidia ubongo kufikia kiwango kikubwa cha kupumzika, pia homoni ya OXYTOCIN humsaidia mwanamke mwenye ujauzito kujifungua kwa usalama zaidi kwani hufanya mfumo wa uzazi kupanuka.
 
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu wengi hasa wazee wanaokumbatiwa mara nyingi huwa na asilimia chache za kukumbwa na magonjwa kuliko wale ambao hawakumbatiwi, hivyo watu hushauriwa kukumbatia wazazi wao kwani hii itawasaidia miili yao kuzalisha kinga ya kupambana na magonjwa.
3 – Kukumbatiana husaidia kupunguza maumivu
 
Madaktari hushauri kuwakumbatia wagonjwa wetu kwani kitendo hicho kidogo kinasaidia ubongo kuachia homoni inayojulikana kama endorphins ambayo husaidia kufunga njia zote katika ubongo ambazo hutuma taarifa ya kuwepo kwa maumivu kwenye mwili.
4 – Husaidia watu kuwa na mood nzuri
 
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu wenye hasira au mood mbaya kila siku huzalisha homoni chache sana za Dopamine na Serotonin ambazo zinasaidia kufanya ubongo kuwa na uchovu na kukosa furaha hivyo kumkumbatia mtu unayempenda inasaidia kuzalisha homoni hizi kwa wingi.
5 – Kukumbatiana huongeza ufahamu kwenye ubongo
 
Watu wanashauriwa kuwakumbatia watu wenye uzito wa kuelewa mambo kwa haraka hasa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa kama Autism na Dementia kwani kitendo hiki husaidia ubongo kuzalisha homoni ya oxytin inayosaidia ubongo kuelewa jambo kwa haraka na kutatua maswali magumu.
6 – Hupunguza msongo wa mawazo
 
Kukumbatiana kunasaidia kupunguza uzalishaji wa homoni inayoitwa Cortiso ambayo husaidia ubongo ku-relax. Homoni hii ikizalishwa kwa wingi kwenye ubongo wa binadamu husababisha hutawaliwa na mawazo hasi yanayopelekea msongo wa mawazo.
7 – Humsaidia mtu kupunguza hofu
 
Tafiti iliyofanywa na Psychological Science Journal imeeleza umuhimu wa kumkumbatia mtu mwenye hofu kwani inasaidia ubongo kupuuza taarifa hasi zinazotumwa kwenye ubongo pia husaidia mtu kuzalisha homoni zitakazomfanya ajiamini.
8 – Huepusha mtu kupata magonjwa ya akili
 
Kukumbatiana kunasaidia kuzalisha kwa wingi homoni ya Dopamine ambapo uzalishwaji wa homoni hii husaidia ubongo kupambana na magonjwa ya akili kama Depression, Bipolar pamoja na Dementia pia homoni hii inasaidia mtu kujiamini na kuwa mkweli.
9 – Husaidia kuepusha magonjwa ya moyo
 
Utafiti uliofanywa North Carolina umesema kuwa watu ambao hawajaonana na wapenzi wao kwa muda mrefu mapigo ya moyo huongezeka kwa mapigo 90 kwa dakika ambapo hali hii sio nzuri kwani binadamu mwenye afya imara hupata mapigo 40 kwa dakika moja.
10 – Husaidia kupumzisha misuli ya mwili
 
Kukumbatiana kunasaidia kupumzisha misuli ya mwili ambapo watu wengi wanapokumbatiana hulegeza misuli yote iliyokaza na kusaidia mwili kupumzika. Hii ndiyo maana wazazi wengi hushauriwa kuwakumbatia watoto wao wanapoamka asubuhi na kabla hawajalala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…