Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matumizi mabaya inatakiwa tuone impact za hao wachezaji
 
Mshambuliaji mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo ameteuliwa na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) kuwania tuzo ya bao bora la msimu. Bao lililomuingiza katika kinyang’anyiro hicho ni lile alilolifunga Real Madrid ilipocheza na Juventus katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Mbali ya Ronaldo wengine wanaowania tuzo hiyo ni mwanasoka wa kike wa England, Lucia Roberta Tough Bronze maarufu kama Lucy Bronze na kiungo chipukizi Elliot Embleton wa Sunderland.
 
Ronaldo alifunga bao hilo kwa shuti kali la tik taka, wakati Bronze, bao lake katika mchezo wa Ligi ya wanawake Ulaya kati ya Lyon ya Ufaransa na Manchester City ya England ndilo lililompatia nafasi ya kuwania tuzo ya bao bora la msimu.

Naye Embleton, bao lake katika michuano ya vijana chini ya miaka 19, kati ya England na Uturuki, huku mpishi wa Tottenham, Christian Eriksen, bao aliloifungia Denmark, katika fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Ireland nalo limeorodheshwa kuwania tuzo hiyo.
 
KWA mara nyingine Wayne Rooney amethibitisha kwamba ng’ombe hazeeki maini baada ya kuendelea kuzifumania nyavu tena kwa mabao ya ajabu huko nchini Marekani. Rooney aliisaidia timu yake ya DC United dhidi Portland Timbers katika ligi ya nchini humo akihusika katika ushindi wa jumla ya mabao 4-1.

Portland walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 35 kupitia kwa Samuel Armenteros. Hata hivyo, Rooney alizisalimia nyavu katika dakika 43 akipokea pasi safi kutoka kwa Yamil Asad kabla ya kuachia shuti kalia lililomshinda mlinda mlango na kuyafanya matokeo kuwa ni 1-1. Kipindi cha pili kilianza kwa mchakamchaka, huku mashambulizi yakiwa ni ya kushtukiza.
 
Hazikupita dakika nyingi tangu kipindi cha pili kianze kwani dakika ya 47 Oniel Fisher akipokea pasi murua ya Luciano Acosta na kufanya matokeo kuwa 2-1. Baada ya goli hilo la kuongoza DC walionekana kuutawala mchezo huku wakifanya mashambulizi makali golini mwa Portland. Dakika ya 67 DC United walifanya shambulizi na hatimaye walinzi wa Portland walimfanyia madhambinje ya eneo la 18.

Hapa ndipo ambapo Wayne Rooney alipewa majukumu ya kupiga mpira wa adhabu. Refa alihesabu hatua zake na kuamuru ukuta usimame alipochora mstari. Rooney akauweka mpira chini na kurudi hatua kadhaa nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…