Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Rooney alifanya kama alivyofanya mara kadhaa akiwa katika Ligi ya Uingereza, aliinama kidogo kisha aliufyatua mguu wa kushoto na kuachia shuti ambalo sio tu liliwapita walinzi wa Portland lakini hata mlinda lango Jeff Attinella aliishia kuugusa tu kwa ncha za vidole lakini hakuuzuia kukwama wavuni dakika ya 68.
 
0EA64981-E3D3-46F1-A567-C3464411737D.jpeg
 
Kilichowavutia wengi na kusababisha uwanja wote wa Audi Field kulipuka kwa kelele huku kila mtu akibaki akishangazwa na uwezo huo wa mkongwe huyo wa soka. Baada ya DC United kupata goli hilo ya 3, presha ilionekana kushuka na kufanikiwa kumilika mpira kwa asimia 55. Hata hivyo zikiwa zimesalia sekunde kadhaa mpira kumalizika DC walijipatia bao la 4 kupitia kwa Darren Mattocvks na kupeleka kilio kwa Portland.
 
Ushindi huu unakuja siku chache baada ya DC United kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Orlando ambapo ilishuhudiwa Luciano Acosta akifunga mabao yote matatu huku akitoa pasi ya bao la ushindi ingawa mechi moja kabla ya Portland walipata sare. Hata hivyo matokeo haya yanaifanya DC United kusalia nafasi ya 8 katika msimu wa Ligi Kuu kuu nchini Marekani.
 
Wayne Rooney aliitamba vilivyo na timu ya Manchester United kabla ya kutimkia katika timu yake ya zamani ya Everton. Hata hivyo alidumu kwa msimu mmoja pekee kabla ya kujiunga na DC United.

Ujio wa Rooney katika ligi ya Marekani unamfanya awe miongoni mwa mastaa waliowahi kuichezea ligi ya nchini humo kwani kuna wachezaji wengine kama Ashley Cole na Zlatan Ibrahimovich amabo wanacheza katika klabu ya LA Galaxy.
 
Back
Top Bottom