Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutegemea msaada kutoka kwa wanaume
Ili kupata mitazamo tofauti, BBC imezungumza na Naibu msajili wa mahakama kuu Tanzania Bi Nyigulila Mwaseba anayesema chuki ni tabia ya mtu tu bila kujali jinsia.
"Si kweli, hii huenda inatokea kwa sababu mtu alitegemea kupata huduma au kusaidiwa na mwanamke mwenzake alafu akakosa hicho alichohitaji ndio mtu husema hivyo. Kwa msimamo wangu naamini mtu yeyote yule anaweza kuwa mwanamke au mwanaume akakufanyia visivyo, anaweza kuwa bosi wako ama vyovyote. Ni moyo wa mtu tu mwenyewe.
 
Kama mtu hana roho nzuri ni yeye tu kwa sababu unaweza kuhudumiwa vizuri na mwanamke mwenzako na ukaudumiwa vizuri na mwanaume pia hii haijalishi. Binafsi naamini ni tabia tu binafsi," anasema Bi Mwaseba.
Hata hivyo anawashauri wanawake hasa wanaokwenda kwenye maofisi mbali mbali kuacha kwenda mahali wakiwa na mategemeo kuwa wakimkuta mwanaume basi watahudumiwa vizuri au ukimkuta mwanamke mwenzako utahudumiwa vizuri. Anasisitiza si vyema kwenda na matarajio.
 
Iwapo umeenda kupata huduma au msaada mahali na mtu uliyemkuta hajakupatia huduma kama inavyotakiwa unaweza kufuata utaratibu wowote ambao utafuata hata kama umemkuta mwanaume na si mwanamke," anaongeza Mwaseba.
Lakini kukinzana mawazo si jambo la kushangaza mwingine anaona ni wivu baina ya wanawake.
 
BBC imezungumza na Shahista Alidina maarufu kama Shaykaa, mwanaharakati wa haki za binadamu. Kwake, tatizo lipo kwa baadhi ya wanawake kukosa kujiamini.
"Unaweza kuta mwanamke amesoma mzuri na ana kila kitu lakini tatizo linakuja kwenye kujiamini, kama unajiamini mwenyewe huwezi kuwa na chuki na mwenzako hata awe amekuzidi vipi kwa sababu unakuwa umejitosha na umeridhika na ulicho nacho na ulivyokuwa sio mwenzio anafanya vizuri unaanza kwanini huyu anaendelea kuliko mimi wakati amekuja juzi tu," anasema Shaykaa.
Hata hivyo Shaykaa anasisitiza kuwa wapo wanawake wengi wanapendana na wanaleta maendeleo kwa pamoja. Na anasisitiza mwanamke ni kujipenda na kujiamini kwani ukiwa hivyo hutapata muda wa kuwa na chuki na mtu.
 
Adui na mshindani
Ni mjadala mkubwa, BBC imezungumza na mwanasaikolojia Sreddie Kyara ambapo yeye anasema kuna tofauti ya adui na mshindani.
"Kisaikolojia nikitazamia adui ni mshindani, naweza kusema mwanamke ni adui mkubwa wa manamke na kwasababu hasa mwanamke hutaka kushindana na zaidi na mwanamke kuliko mwanaume kwa hiyo hii ndio inapelekea kufanya mwanamke kuwa adui mkubwa wa mwanamke kuliko mwanaume kuwa adui wa mwanamke," anasema Kyara.
Hata hivyo anasisitiza kuwa maumivu mengi ya wanawake husababishwa na wanawake wenzao pamoja na kwamba wanaume hushiriki. Anatolea mfano wa mahusiano kuwa mwanamke huyu huyu anatembea na mume wa mwenzie akijua wazi kuwa mwanamke mwenzake ataumia na kuteseka.
 
Kama wanawake wangeungana wakasema wanataka kukomesha mateso wanayopitia wangefaulu sana. Lakini kwa sababu mateso mengi wanawake wanayopitia ni kwa sababu wanawake hao hao wanaruhusu wanaume kuwafanyia wanawake wenzao ni ngumu," anaongeza Kyara
Hata hivyo mwanasaikolojia huyo amewataka wanawake kuamka ili kumaliza ushindani na wakati huo huo amewasifu wanawake kuwa wana bidii ya kusaidiana.
"Wanaowasaidia wanawake kwa asilimia kubwa ni wanawake na kwa msaada ambao ni halisia ni wanawake kuliko wanaume, lakini pia wanawake watambue kuwa atakayeweza kumuinua mwanamke ni mwanamke mwenyewe na atakayeweza kumwangusha mwanamke kwa nguvu zaidi si mwanaume ni mwanamke mwenzake," Kyara ameiambia BBC.
Bila shaka huu ni mjadala mzito ambao ni vigumu kufikia tamati, wewe una maoni gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…