Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ARSENE Wenger amepigwa chini, lakini bado Arsenal imeendelea kuwa wepesi pindi inapokutana na wababe wenzake wa Top Six kwenye Ligi Kuu ya England.
Imekubali tena kipigo cha mabao 3-2 mbele ya Chelsea ikiwa ni cha pili baada ya kupigwa 3-0 na Manchester City kwenye mechi ya ufunguzi iliyopigwa uwanjani Emirates.
Mashabiki waliamini kuwa Profesa Arsene Wenger ameishiwa mbinu za kupambana na makocha wenye damu change kama Pep Guardiola na Jose Mourinho, hivyo wakapambana na kuletewa Emery Unai kutoka PSG ya Ufaransa.
Hata hivyo, mambo bado ni magumu na Arsenal wamepoteza mchezo wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya England.
 
Kinachowaumiza zaidi mashabiki wa Arsenal ni kwamba, wamefungwa mechi zote na timu za Top Six ambazo zinawania ubingwa na nafasi za juu kwenye msimamo.
Katika mchezo wa jana uliopigwa kwenye dimba la Stamford Bridge jijini London, Chelsea ilianza kufungua akaunti ya mabao kupitia kwa Pedro Rodriguez katika dakika ya tisa tu kabla ya Alvaro Morata kupachika la pili dakika ya 20.
Mabao ya Chelsea yalitokana na kazi nzuri ya Willian na beki wa kushoto, Marcos Alonso ambaye alikuwa akipanda na kushuka na kusumbua ngome ya ulinzi ya Arsenal iliyoonekana kutokuwa na maelewano mazuri.
 
Hata hivyo, Arsenal walitulia na kutengeneza mashambulizi langoni mwa Chelsea, lakini washambuliaji wake hawakuwa makini kwa Pierre Aubameyang na Henrikh Mkhitaryan kushindwa kumalizia nafasi za wazi.
Lakini, makossa hayo hayakuwavunja nguvu Arsenal na dakika ya 37 Mkhitaryan alibadili matokeo na kuwa 2-1 baada ya kumalizia krosi ya Aubameyang ambayo Willian alizembea kuokoa kabla ya Alex Iwobi kuisawazishia Arsenal dakika tatu kabla ya mapumziko na matokeo kuwa 2-2.
 
Hata hivyo, wakati Arsenal wakiamini mchezo huo unaweza kumalizika kwa sare ya 2-2, Alonso alizamisha jahazi la Emery kwa kupachika bao la tatu na kupeleka kilio Emirates.
Kwa matokeo hayo, Chelsea inayonolewa na Maurizio Sarri ina pointi sita baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo, ambapo awali ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Huddersfield.
 
CHELSEA: Kepa, Azpilicueta, Rudiger, David Luiz, Alonso, Jorginho, Kante, Barkley, Willian, Pedro, Morata.
ARSENAL: Cech, Bellerin, Sokratis, Mustafi, Monreal, Guendouzi, Xhaka, Iwobi, Ozil, Mkhitaryan, Aubameyang.

MATOKEO MENGINE
Cardiff City 0-0 Newcastle United
Chelsea 3-2 Arsenal
Everton 2-1 Southampton
Leicester City 2-0 Wolves
Tottenham 3-1 Fulham
West Ham 1-2 Bournemouth2
 
STRAIKA matata na fundi wa kupasia nyavuni wa Tottenham, Harry Kane amemaliza ukame wa mabao akifunga bao lake la kwanza kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu England.
Kane, ambaye aliibuka Mfungaji Bora kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 kule Russia, alipachika bao hilo kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Fulham katika Uwanja wa Wembley.
Katika mchezo huo, mabao mengine ya Tottenham yalifungwa na Kieran Tripper na Lucas Moura. Huu ni ushindi wa pili kwa Spurs baada ya kuichapa Newcastle United manbao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza, ambao Kane alitoka kapa.
 
Hata hivyo, kufunga bao hilo sio ishu kubwa kwa Kane, lakini benchi la ufundi, mashabiki na wachezaji wenzake wamepatwa mzuka kutokana na staa huyo kuwa na gundu unapoingia mwezi huu wa Agosti.
Rekodi zinaonyesha kuwa, Kane amekuwa akikumbana na wakati mgumu wa kupasia nyavuni kila unapofika mwezi kama huu hivyo, bao hilo limepokewa kwa furaha kwelikweli klabuni kwake.
 
Cristiano Ronaldo
Supastaa mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo jana alianza kuichezea timu yake mechi ya kwanza ya Serie A huku wakichomoza na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Chievo ugenini. Hata hivyo, kwenye mchezo huo, Ronaldo amemaliza dakika 90 bila kufunga bao.
 
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anatumia mbinu ile ya ‘mchawi mpe mwana amlee’ kwa kiungo Mfaransa Paul Pogba.
Hiyo imetokana na uamuzi wake wa kuendelea kumpa kitambaa cha unahodha Pogba katika mechi ya Ligi Kuu itakayochezwa ugenini kesho dhidi ya Brighton.
Mourinho alimpa unahodha Pogba katika mchezo uliopita walipocheza na Leicester City na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku Pogba akifunga bao la kwanza.
 
Katika mchezo huo kiungo huyo alicheza kwa kiwango cha juu licha ya kuaminika kuwa na kinyongo na ameshamwambia wakala wake Mino Raiola amfanyie mipango ya kuhama.
Wakala huyo alifanya mazungumzo na kina na kuafikiana na Barcelona lakini United, wakautolea nje uhamisho huo.
Akizun gumza jana jioni Mourinho alisema anamuamini Pogba na kwa kuthibitisha kuwa hana tatizo naye anampa tena kitambaa cha unahodha katika mchezo wa kesho.
Uhusiano wa Mourinho na Pogba haupo vizuri kwa muda sasa Kocha huyo amekuwa akimshambulia kiungo huyo kwamba anacheza chini ya kiwango kwenye klabu tofauti na anapokuwa kwenye timu ya Taifa.
Pogba alikuwa mmoja wa wachezajki walioiwezesha Ufaransa kutwaa ubingwa wa Dunia Julai mwaka huu kwa kufunga bao la tatu katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Ctoaria katika fainali.
 
Ukiwasikia wachezaji wa Chelsea wanavyosema kuhusu kocha wao mpya Maurizio Sarri utajua jamaa kawatia ndimu.
Asubuhi Sarri aliwasili katika viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo vilivyopo Cobham jijini London na kuwapa mazoezi mepesi vijana wake.
Beki huyo wa zamani wa kitaliano mwenye miaka 59, akijua kuwa leo ana mechi ngumu mbele yake dhidi ya Arsenal aliwapa wachezaji mazoezi mepesi lakini yeye mwenyewe akiwaongoa kwa kuwapa mifano.
 
Jambo hilo limewakuna wachezaji na kuanza kuhoji kwa nini Kocha huyo amechelewa kutua Stamford Bridge.
Sarri alianza ‘kuwatia ndimu' wachezaji wake tangu jana, wakati wa mazoezi akiwaambia kuwa wakitaka wanaweza kuifunga Arsenal idadi yoyote ya mabao ila wasipotaka wanaweza kutoka nayo sare.
Akifafanua alisema wakicheza kama anavyowaelekeza yeye wataifunga mabao mengi ingawa yeye anataka washinde mabao 3-0, akisema kwa mfumo wake kuna bao linatengenezwa ndani ya kila dakika 15.
Wachezaji wamemuahidi kutekeleza hilo kwa kiapo baada ya kocha huyo kujitia kitanzi kwa kuahidi kuwapa zawadi ambayo hakuitaja iwapo watatimiza ahadi hiyo ya kufunga Arsenal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…