Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sarri kama ilivyo kwa Emery, huu ndio msimu wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu England, lakini ameonekana kuanza vizuri tofauti na mwenzake huyo.

Kocha Emery amepoteza mechi zote mbili, ambapo alianza kwa kuchapwa na Manchester City mabao 2-0 kisha akalala kwa Chelsea 3-2.
 
KIWANGO cha kiungo wa fundi wa Kijerumani, Mesut Ozil kimezidi kuwavuruga wengi na sasa supastaa wa zamani wa Arsenal, Nwanko Kanu amejivisha mabomu na kuingilia kati.

Kanu, ambaye amekuwa kimya huku Ozil akiendelea kukosolewa akidaiwa kucheza chini ya kiwango hasa kwenye mechi kubwa, sasa ameamua kimwaga ugali.

Mpachika mabao huyo aliyecheza kwa mafanikio Arsenal, amewataka mabosi wa klabu yake hiyo kuamua moja kumuacha Ozil acheze mpira wake ama wamuweka sokoni.

“Hivi unaweza kumwambia Messi au Maradona arudi nyuma kukaba?” Alihoji Kanu.

Kwa mujibu wa Kanu, amewataka Arsenal kukubaliana na staili ya uchezaji wa Ozil kwa kuwa hawezi kubadilika na wakiona ni tatizo zaidi basi wamuuze.

Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa klabuni Arsenal akipokea Pauni 300,000 kwa wiki na hilo limekuwa likimfanya kuwa kwenye matatizo kila timu inapopoteza mchezo.

Hata hivyo, Kocha wa Arsenal Unai Emery, amekuwa akijaribu kuzungumza na Ozil na kumtaka kutimiza majukumu yake uwanjani ili kusaidia timu kupata matokeo bora.

Lakini Kanu amemshauri Emery kumpa Ozil majukumu ya kuchezesha timu zaidi kwa kuwa, ndio eneo analolidumu zaidi na hapo ataona matokeo.
 
Kiungo wa Daniel Arzani, mwenye miaka 19, anaamini kutolewa kwa mkopo kwenda kuichezea klabu ya Celtic kutamsaidia kujiweka sawa ili kuija kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Manchester City (Manchester Evening News)
 
Chelsea iko tayari kusikiliza ofa itayokuja klabuni hapo ikimtaka mchezaji wa kiungo Danny Drinkwater, ambae ameanza katika michezo mitano tu ya msimu uliopita akiwa amesajiliwa kwa kiasi cha pauni 35 akitokea Leicester City (Mail on Sunday)
 
Manchester City wameambiwa watalazimika kuilipa Borussia Dortmund's kiasi cha pauni milioni 68, kama inataka kumsajili kiungo Julian Weigl, ambae pia anawindwa na miamba ya soka ya Ufaransa Paris St-Germain (France Football, via Sun on Sunday)
 
Bosi wa zamani wa vilabu vya Everton, Manchester United, Sunderland na West Ham David Moyes anaongoza mbio za kupewa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani (Sunday Times - subscription only
 
Klabu ya Barcelona imekubali kuwa timu ya Manchester United haitomuuza kiungo wake Mfaransa Paul Pogba, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili tarehe 31, mwezi huu, ila wataangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo dirisha lijalo la usajili . (Sunday Express)
 
Kiungo wa Wolves Mreno Ruben Neves mwenye miaka 21 ameingia kwenye rada za Manchester City na klabu hiyo inataka kumsajili mchezaji huyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari kwa dau la pauni milioni 60(Sun on Sunday)
 
City's Fantom claims to be 'the world's first football smartband' and supporters can buy the sky blue device from Monday for £79.99.

The wristband informs fans on the countdown to kick-off, live match details and breaking news as well as giving them the chance to have their say and play quizzes.
 
The club released a video of fans wearing the bands and giving their thoughts on the new concept.

One fan said: 'It keeps you much closer to the club, you get instant news, stats and information about the club.'

Another added: 'It's here in an instant on your wrist, you don't have to get your phone out of your pocket.
 
While another supporter said: 'The best thing I've ever seen from Manchester City, brilliant.'

The introduction of the new technology has also created a reaction on social media.

One Twitter user wrote: 'They are so try hard it's not even funny anymore.'

While another added: '£80 for free news... what a joke.'

One Tweet read: 'Awful idea. Why not have updates through smart watch or an app? Creating another piece of tat for people to wear. What's the point?'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…