Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miongoni mwa wanakikundi hicho ndipo hupatikana viongozi wa kukisimamia kikundi hicho au shirika hilo katika mchakato mzima wa usajili, kuanzia na mapendekezo ya majina ya Shirika, kuandaa vikao vya shirika.

Usajili wa mashirika haya hutofauitiana kulingana na ngazi husika ya utekelezaji wa shughuli za shirika husika.Shirika linaweza likasajiliwa na kufanya kazi katika ngazi ya kata, ambapo katika ngazi hii ofisa mtendaji wa kata husika ndiye atakayehusika na usajili huu kwa kutoa vibali maalumu.
 
Katika ngazi ya wilaya, mkuu wa wilaya husika ambapo shirika hili litafanya shughuli zake ndiye anayebeba dhamana ya usajili wa shirika hilo. Vilevile katika ngazi ya mkoa, mkuu wa mkoa husika atahusika na usajili wa shirika hilo, lakini katika ngazi ya taifa au kimataifa, Wizara itahusika na usajili wa shirika. Ni lazima ifahamike kuwa kuendesha shirika pasipo kusajiliwa ni kosa kisheria.
 
Wakati wa usajili wa shirika la namna hii ni muhimu sana mambo yafuatayo yakazingatiwa ili kuweza kukamilisha mchakato wa usajili; Katiba ya shirika nakala 3 zilizofungwa vizuri – ambayo ndani yake kutakuwa na malengo ya shirika, maono ya shirika na mbinu za utekelezaji wa maono hayo. Ndani ya katiba pia itaeleza idadi na aina ya mikutano ya Shirika, muda wa viongozi kukaa madarakani na namna ya mapato na matumizi ya fedha na rasilimali za shirika, namana kutatua migogoro n.k
 
Wasifu wa viongozi (CV), ifahamike kuwa uimara na uadilifu wa viongozi ndio nguzo imara ya maendeleo na mafanikio ya Shirika, hivyo ni lazima wajumbe wote wa Shirika watafakari kwa kina uwezo wa viongozi wanaowachagua au kuwateua kuliongoza Shirika. Japo wazo la kuanzisha shirika hutoka kwa mtu mmoja mwenye maono lakini si lazima mtoa wazo akawa sehemu ya uongozi. Barua ya utambulisho kutoka ofisi ya mkuu wa Wilaya, barua hii ni muhimu sana katika usajili wa Shirika hasa ngazi ya Kitaifa, barua hii humaanisha kuwa shirika linatambulika kuwepo na kufanya shughuli zake katika Wilaya husika. Barua ya kuomba kusajiliwa kwa Shirika, ni vyema kufahamu kuwa Shirika pia linatakiwa kuwa na barua yake ya kuomba kusajiliwa, na anuani ya barua iendako itategemea na ngazi ya ambayo Shirika linakwenda kusajiliwa. Fomu ya usajili wa shirika (NGO A – Form No.1), hii ni fomu kuhusiana na usajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali. Fomu hii itapaswa kujazwa kikamilifu na kusainiwa na mwenyekiti na katibu wa Shirika husika.
 
Majina pendekezwa ya shirika yasiyopungua matano na Ada ya Usajili. Majina haya husaidia kutumika kama majina mbadala pale inapotokea baadhi ya majina kufanana na majina ya mashirika mengine yaliokwishasajiliwa au kukataliwa kutokana na sababu nyinginezo za kiutawala na kimaadili). Malipo ya Ada ya usajili ndio kielelezo kuwa mchakato wa usajili umekubaliwa na cheti kinaelekea kutolewa.
 
Uwepo wa Kitambi mwilini ni kiashiria kimojawapo cha unene na ndiyo maana wataalamu wa afya hupima mzunguko wake kama moja ya njia ya kutathimini tatizo la unene.

Kitambi hujulikana pia kama kiribatumbo ni matokeo ya ulaji holela wa vyakula na kutoushughulisha mwili na mazoezi au kazi.

Wapo wanaokosa muda wa mazoezi kutokana na majukumu ya kazi na wengine kukosa maeneo ya mazoezi ili kukabiliana na vitambi.
 
Je unahitaji shilingi ngapi na eneo kubwa kiasi gani ili tu kumiliki kamba na kufanya zoezi la kuruka kamba?

Kuruka kamba ni moja ya zoezi rahisi lenye faida ambalo watu wengi hawalizungumzii kabisa kama ni moja ya kundi la mazoezi mepesi kitaalamu hujulikana kama aerobics exercise.

Kamba ya kisasa inapatikana kwa wafanya biashara ndogondogo kwa bei isiyozidi Sh10,000. Ina vishikilio ambavyo inarahisisha kuikunja vizuri na kuihifadhi katika begi la kiofisi au kazi.
 
Unahitaji dakika 15-20 kwa siku mara tano kwa wiki na eneo lenye ukubwa wa futi 4 kwa 6 kufanya zoezi hili linalokadiriwa kuchoma kiwango cha nishati kalori 10-15 kwa dakika.

Zoezi hili linafaida kubwa kiafya ikiwamo kukata kitambi, kuimarisha mfumo wa moyo na damu, hewa (mapafu), fahamu (ubongo) na kujenga misuli imara.

Ukiwa nyumbani, ofisini, vituo na viwanja vya wazi vya michezo ruka kamba eneo tambarare ukiwa umavaa raba ili usijijeruhi. Ongeza hamasa ya zoezi na mziki wa haraka haraka toka katika simu yako.

Kabla ya kuanza nyoosha kwanza viungo angalau kwa dakika 5 kisha jikadirie urefu wa mzunguko wa kamba na anza kuruka taratibu na baadaye ongeza kasi.
 
Ukiruka kamba kwa ufasaha na kujituma unaweza kuchoma kiwango kikubwa cha mafuta mwilini pengine kuzidi kile cha zoezi la kutembea au kukimbia umbali mrefu.

Tafiti zilizofanywa na Chuo kikuu cha Havard na kuchapishwa katika jarida la Science Daily zinaonyesha zoezi hili likifanywa dakika 30 kwa siku linawezesha viungo vingi mwilini kushughulika kikamilifu.

Hii ni faida kiafya kwani mafuta yaliyorundikana ikiwamo ya kiriba tumbo huchomwa na hivyo kukuepusha na magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo ya Moyo, Kisukari, Kiharusi, Figo na Unene.
 
Kama utahitaji kujiweka fiti zaidi unaweza kuruka kamba dakika 30 zaidi kwa mfululizo na wale wanaoanza kujifunza watumie dakika 10 kwakuachana mpaka watakapozoea.

Zoezi hili lina tija sana ndiyo maana linapendelewa na mabondia wengi duniani kwasababu linawafanya kuwa na stamina, pumzi , wepesi na misuli imara yenye nguvu.

Litumie zoezi hili kupata matokeo makubwa kiafya kwani ni rahisi kufanyika na halihitaji gharama ukilinganisha na mengine.

Kufanya mazoezi ni kama wito kwa muhusika, inakuwa ngumu kufanya mazoezi kwa kujishauri, Kikubwa ni kuamua sasa ninafanya mazoezi haya kwa kutengeneza ratiba maalumu ya kila siku badala ya kuwa na ratiba yenye mapengo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…