mambo ya msingi katika mahusiano. Hapa utapata tafakari ya maana ya maneno naimani ambazo zinatutatiza wengi wetu. 1. Mchanganyiko mkubwa kuhusu maana yamahusiano, mapenzi na ndoa: Labdakipengele hiki tuanze kwa kueleza kuwa kunaweza kuwepo ndoa, lakini yasiwepomahusiano... wala mapenzi. Inaweza kuonekana kama inachanganya kidogo, lakini ndioukweli wenyewe. Ndoa ni namna tuu ambayowawili walio kwenye
mahusiano wanaamua kuwataarifu rasmi watu wengine kuwa waowapo rasmi katika mahusiano. Ndoa ni kiapo mbele ya watu wengine , na ni namnaya kutaka kumuhakikishia mwenza wako kuwa endapo kiapo hicho kitatokeakuvunjika, basi unakubali rasmi kuwajibika kwa mujibu wa taratibu zilizopo zandoa husika, ikiwemo kukubali kuitwa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kugawanamali, n.k. Na kwa upande wa kiroho, inabeba maana zaidi kuwa unaweka kiapo kwaMungu wako kuwa utalinda mahusiano yako na huyo unayemchagua. Hivyobasi, ndoa haijengi mahusiano wala mapenzi.