Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yafuatayo ni matokeo ya Ligi Kuu 5 duniani



ENGLAND

Wolves 1 - 1 Man City

Bournemouth 2 - 2 Everton

Arsenal 3 - 1 West Ham

Huddersfield 0 - 0 Cardiff City

Southampton 1 - 2 Leicester City

Liverpool 1 - 0 Brighton
 
UJERUMANI

Bayern Munich 3 - 1 Hoffenheim

Fortuna D 1 - 2 Augsburg

Hertha Berlin 1 - 0 Nuernberg

Freiburg 0 - 2 E.Frankfurt

Wolfsburg 2 - 1 Schalke 04

Werder Bremen 1 - 1 Hannover 96

B.M'ngladbach 2 - 0 B.Leverkusen
 
LIGI Kuu England haina ubishi kwamba ndiyo ligi inayotoa burudani zaidi hapa duniani. Ubingwa wa Ligi Kuu England umekuwa wa mchakamchaka kweli kweli. Kutokana na hilo, ndio maana kumekuwa na rekodi hizo ambazo unaweza kuziona kama si za kweli vile, lakini ni ukweli mtupu.
 
7.Shearer akosa penalti nyingi

Anashikiria rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi Kuu England baada ya kutupia wavuni mara 260. Anashikilia rekodi ya kufunga hat-trick nyingi na penalti nyingi, akifunga mara 56. Lakini, Alan Shearer ndiye mchezaji anayeshikilia pia rekodi ya kukosa penalti nyingi kwenye Ligi Kuu England baada ya mshambuliaji wa zamani wa Newcastle United Blackburn Rovers kushuhudia akikosa mikwaju 11 ya penalti hizo.
 
6.Medali za burebure

Kwenye Ligi Kuu England kuna mchezaji mmoja aliitwa Richard Wright. Staa huyo kwenye rekodi zake alicheza mechi 12 kwenye Ligi Kuu England kwenye kikosi cha Arsenal na Manchester City. Lakini, Wright mechi zake zote hizo alicheza kwenye kikosi cha Arsenal na huko Man City hakucheza mechi yoyote kwenye ligi, lakini bado alipata medali mbili wa ubingwa. Kipa huyo alibeba ubingwa na Arsenal na kisha akabeba akiwa na Man City, licha ya kwamba alipokuwa Etihad alikuwa akisugua tu benchi. Steven Gerrard kwa kucheza kote tena kwa jitihada kubwa alipokuwa na Liverpool, lakini hajawahi kushinda medali ya ubingwa wa Ligi Kuu England.
 
5.Siku nyingi mkiani bila kushuka daraja

Wanasema hivi, kama ipo, ipo tu. Leicester City walikuwa kwenye wakati mgumu wa kukwepa wasishuke daraja mwaka 2014, lakini kwa miaka miwili iliyofuatia tu, wakabeba ubingwa wa Ligi Kuu England. Katika msimu wa 2014/15, Leicester City walitumikia sehemu kubwa ya msimu wao wakiwa mkiani wakipambana wasishuke daraja. Timu hiyo ilikaa mkiani kwa siku 140, lakini hawakushuka. Leicester City walizidi kuwashagaza watu baada ya kwenda kubeba ubingwa msimu uliofuatia, 2015/16 walipokuwa chini ya kocha Claudio Ranieri.
 
4.Penalti miguu yote

Ni kitu kitakachokuwaza kinywa wazi kwa maana ya kuona mchezaji mmoja akiamua kupiga penalti kwa miguu yote miwili. Lakini, kwenye Ligi Kuu England kuna wachezaji wawili waliojaribu kufanya hivyo na kufunga penalti zao walipopiga kwa miguu ya kushoto na miguu ya kulia. Washambuliaji Bobby Zamora na Obafemi Martins ndiyo wachezaji pekee waliofunga penalti zao kwenye Ligi Kuu England walipopiga kwa miguu yote miwili. Ni rekodi tamu kinoma.
 
.Giggs aongoza kwa kufanyiwa sub

Gwiji wa Manchester United, Ryan Giggs ameshuhudia rekodi yake ya kucheza mechi nyingi kwenye Ligi Kuu England ikivunjwa na veterani wa West Brom, Gareth Barry. Lakini, mkongwe huyo wa zamani wa Old Trafford bado anashikilia rekodi nyingine matata kabisa. Giggs ndiye mchezaji aliyefanyiwa sub mara nyingi kwenye historia ya Ligi Kuu England baada ya kufanyiwa hivyo mara 134.
 
2.Rooney afunga, ajifunga

Staa, Wayne Rooney ameingia kwenye orodha ya wachezaji watatu, pamoja na Gareth Bale na Kevin Davies kwa kufunga, kujifunga na kutoa asisti katika mechi moja ya ligi. Kitu ni kitu nadra sana kutokea kwa mchezaji na ndio maana tangu Ligi Kuu England ni wachezaji hao tu watatu ndio walioweka rekodi hiyo ya kufunga, kujifunga na kuasisti katika mechi moja. Rooney amecheza mechi 770 amefunga mabao 328 na kubeba mataji 16, huku akiwa kinara wa muda wote wa mabao Manchester United na England.
 
1.Balotelli ana asisti moja tu

Supastaa, Mario Balotelli ameshawahi kucheza kwenye Ligi Kuu England akipita kwenye klabu za Manchester City na Liverpool. Kwa ujumla, straika huyo Mtaliano amecheza mechi 70 za Ligi Kuu England, lakini kitu cha kushangaza amepiga asisti moja tu, ile ya bao alilofunga Sergio Aguero na kuwapa ubingwa Man City walipoichapa QPR mwaka 2012 kwenye mechi ya mwisho ya msimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…