Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nchi Kongwe kwa Ustaarabu Duniani ni Misri.

Misri ya kale yakadiriwa miaka 3,000 iliyopita ndiyo jamii kubwa iliyostaarabika kutokea Duniani. Wamisri waliishi kandokando ya mto Nile na kitamaduni walistaarabika katika namna wanavyoongea, wanavyoabudu, wanavyoelewa na kuchukulia ulimwengu wa kaisili, walivyojiendesha kwa serikali mbalimbali, walivyoishi, walifanya matukio ya kijamii na burudani mbali mbali, na jinsi walivyojihusisha na wengine ambao hawakuwa wamisri.
 
Unapomkuta mwanamke au mwanaume ambaye yuko kwenye ndoa, amevua au huwa anavua pete yake ya ndoa mara kwa mara na kuiweka kwenye mkoba wake au mfukoni, utasemaje?

Ni lazima kuna namna ambayo utamfikiria mtu huyo. Je, utamfikiria kwamba ni malaya, haridhiswi na ndoa yake, au hampendi mumewe au mkewe?

Hapa nitajaribu kutoa maelezo ambayo, yatakufanya usihisi vibaya kwa kile ambacho, umekuwa ukikifikiria kuhusu mwanamke au mwanaume wa aina hiyo.
 
Imeelezwa kwamba, wale wanawake au wanaume ambao, huficha pete zao za ndoa, ni watu ambao hawana uwezo wa kulea watoto, yaani huwa wanawapuuza sana watoto wao.
Kwa kulinganisha, inaelezwa kwamba, wale wanawake au wanaume wenye kuvua au kupenda kuvua pete zao za ndoa na kuziweka mikobani, huwa wanawapuuza watoto wao kuliko wale ambao, huvaa pete zao muda wote.

Lakini pia, inaelezwa kwamba wale wanawake au wanaume wenye sura za kuvutia au nzuri sana wanapokuwa na tabia hii ya kuficha pete zao za ndoa, huwa ni wazazi wasioweza hata chembe kulea watoto wao, yaani wanakuwa ni wazazi aambao, ni watekelezaji sana, wasiojali kabisa kuhusu watoto wao.
 
Katika moja ya tafiti zake mwanasaikokoljia Andrew Harell wa chuo kikuu cha Alberta nchini Canada, anasema kwamba, hili sio suala la kubahatisha, kwani amelifanyia utafiti kwa wengi, kwa muda mrefu na katika mazingira tofauti.

Mwanasaikolojia huyo anazidi kudai kwamba, hata linapokuja suala la kuangalia na kutunza wagonjwa, wale watu wanaoficha pete zao za ndoa, hawana uwezo wa kuwatunza wagonjwa ukilinganisha na wale wenye kuvaa pete.
 
Inaelezwa kwamba, kuvua pete ya harusi na kuificha ni ishara kwamba, mwenye pete hiyo hana hisia au uwezo wa kujifunga na ndoa yake au familia yake. Kwa kukosa sifa hizo, ni wazi mtu huyo hawawezi kujifunga na watu wengine wenye kuhitaji msaada wake wa kihisia kama vile wagonjwa.

Kuvua au kuficha pete ya ndoa, kunahesabiwa kama ni dalili ya mtu kutaka kuanzisha uhusiano mpya nje ya ndoa yake. Haja hiyo inapotimizwa, uwezekano ni mkubwa kwa mwanaume au mwanamke kupunguza upendo au kujali familia yake, akiwemo mke au mume au watoto. Kwa hali hiyo, kuficha pete ni dalili ya kutokujali na kushindwa kujifunga kwenye uhusiano
 
Wakati huo huo taarifa za kitafiti zinaonyesha kwamba, wazazi wenye kuvua pete huwa hawatoi uangalifu mkubwa kwa watoto wao wenye sura mbaya, ukilinganisha na ule wanaoutoa kwa watoto wao wenye sura za kuvutia au wazuri.

Katika moja ya tafiti zilizowahi kufanywa, zilihusisha wazazi na watunza watoto walioenda na watoto hao kwenye supermarkert. Ilionekana kwamba, wale watoto wasiopendeza, waliachwa kwa umbali mkubwa bila wazazi wao kujali, wakati wale watoto wenye kuvutia, wazazi au walezi walikuwa nao karibu sana.
 
Tafiti zote hizo zinajaribu kuonyesha upo uhusiano mkubwa sana kati ya kitendo cha kuvua pete na suala zima la kujali. Je, hali hiyo kwako ikoje? Huu ni utafiti tu, wewe je, unasemaje?
 
Johnny Depp na Vanessa Paradis
Mwigizaji Johnny Depp na mpenzi na mwimbaji wake wa zamani, Vanessa Paradis, wanasemekana hawapendi kuoga. “John huwa ananuka kwani huoga mara chache sana,” kinasema chanzo kimoja cha Fox News na kuongeza kwamba na Vanessa yake yuko hivyohivyo, na kwamba walikuwa wamekutana watu wasiopenda afya zao.
 
Robert Pattinson
Mwanamuziki, mwanamitindo na mwigizaji huyo hivi sasa ni msafi kidogo ambapo anasemekana hapo nyuma alikuwa ananuka vibaya. Alipoulizwa na shirika la habari la Extra iwapo kweli alikuwa hajaweka mafuta kwenye nywele zake kwa majuma kadhaa, alijibu kwamba hajui. Akaongeza: “Sioni maana ya kusafisha nywele. Sioni pia haja ya kusafisha nyumba yangu; sijali.”
 
Zac Efron
Mwigizaji huyo si mpenzi wa kuoga pamoja na kwamba huwa anacheza mpira wa kikapu. “Zac si shabiki wa kuoga, akimaliza kucheza huendelea na maisha bila kwenda bafuni,” kinasema chanzo.
 
Leonardo DiCaprio
Mwigizaji na prodyuza wa filamu, Leonardo DiCaprio, anasemekana anapenda sana mazingira kiasi kwamba hataki maji yatumike ovyo kwani yanasaidia kuotesha mazingira. Yeye huoga mara chache kwa siku na hapendi manukato akisema hayana uasili wowote. Kutokana na kuwa katika hali hiyo, nyumba yake na yeye mwenyewe hutoa harufu mbaya.
 
Cameron Diaz,
Mwigizaji Cameron Diaz, hapendi kutumia pafyumu akisema zinanuka, hasa zikipuliziwa kwenye kwapa zisizonyolewa. Diazi anasema hajatumia pafyumu kwa karibu miaka 20 kwa vile hunuka vibaya. Anasema: “Dawa ni kunyoa makwapa ili kuondoa harufu ambayo hubakizwa humo na pafyumu.”
 
Julia Roberts
Mwigizaji huyo pia anasemekana huwa ananuka. Kisa? Hapendi kutumia pafyumu kwa vile anasema hicho si kitu anachokipenda. Inasemekana pia Julia hapendi kabisa kuoga kila mara, anaweza kukaa siku kadhaa bila kuoga. Badala yake anapenda maji yatunzwe kwa ajili ya mazingira. Isitoshe, anapenda kusikia harufu yake ya mwili yenye mafuta ya asili na hapendi kuziosha nywele zake kila mara kwani ni ngumu mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…