*Bado haijawa proved kwamba alijirusha mwenyewe, tunaendelea na upelelezi wakati tulipoenda kukagua eneo la tukio tulikuta pochi yake ikiwa na simu ambapo hatukuzikuta line zote mbili kwenye simu hiyo lakini pia simu moja na line yake havionekani kabisa, pili inasemekana aliwasiliana na mkurugenzi mkuu kwa njia ya E-mail kuwa akakabidhi document za ofisi ambazo bado zilikuwa mikononi mwake cha kushangaza documents zinakabidhiwa saa kumi usiku?, tumeenda kukagua cctv camera kuna baadhi ya matukio haonekani mfano ilifika sehemu Sr. anapanda ngazi mara ghafla akapotea mpaka tukashtuka nikiwa na Rco, kwa kweli ni mambo ya ajabu tulioyaona. Na ukumbuke pia kabla tulikuwa tunapeleleza upotevu wa zaidi ya Tshs. Milioni 500, ambapo yeye alikuwa mkuu wa idara ya fedha lakini katika uchunguzi wetu tuligundua watu wa chini yake ndio waliohusika kupiga hizo hela kwa kufungua akaunti tofauti na zile za hospitali. Lakini vilevile ikumbukwe BMC inamilikiwa na Kanisa katoliki na serikali pia hivyo kuna pande mbili za uongozi na inavyosemekana hizi pande mbili hazikuwa na maelewano mazuri. Kitendo cha Sister huyu kudondoka kutoka katika corridor ya ghorofa ya tatu karibu kabisa na dirisha la mkurugenzi mkuu ambaye yuko upande wa serikali pia imeleta maswali mengi ya kujiuliza. Hiyo ndio taarifa ambayo naweza kuwajulisha kwa sasa, tuacheni tufanye upelelezi then tutakuja na taarifa kamili*
Tunapofanya mazoezi ya kila siku au kushiriki mashindano mbalimbali ni kawaida mwili kupata majeraha madogo madogo, ya kati mpaka makubwa ambayo yanatupa maumivu na homa.
Majeraha hayo yanaweza kuwa ya tishu laini ya wazi yenye mchaniko ama michubuko au kidonda, yanaweza kuwa butu yasiyo ya wazi, ya kuvunjika au kuteguka na pia yakawa mchanganyiko wa vyote.
Mambo 10 yafuatayo yanaweza kufanywa na majeruhi wa michezo ili kuongeza kasi ya uponaji wa majeraha kwa wakati.
Moja, kuacha mara moja kufanya mazoezi au shughuli zozote zinazoweza kusababisha kujitonesa, kujijeruhi au kupata jeraha jipya. Kupumzika sehemu salama na kulala masaa 6-8 kwa usiku mmoja.
Mbili, kushikamana na ushauri na matibabu ikiwamo matumizi sahihi ya dawa za mumivu, zakuzuia maambukizi na matumizi ya vidonge vya virutubisho maalum.
Tatu, utulivu wa kiakili unahitajika kwani shinikizo la kikakili au msongo wa mawazo huathiri kinga ya mwili ambayo ndiyo nguzo muhimu katika kukarabati na kulinda jeraha. Epuka mambo yote yanayokutikisa kiakili.
Nne, kuzingatia maonyo na makatazo yote ikiwamo mitindo mibaya kimaisha kama vile ulevi wa pombe, matumizi ya tumbaku na dawa za kulevya kwani vinaudhoofisha mwili na kuchelewesha uponaji.
Nne, kuzingatia maonyo na makatazo yote ikiwamo mitindo mibaya kimaisha kama vile ulevi wa pombe, matumizi ya tumbaku na dawa za kulevya kwani vinaudhoofisha mwili na kuchelewesha uponaji.
Tano, kuzingatia usafi wa mwili ili kuepukana na uvamizi wa vimelea vya maradhi mengine ambayo uwepo wake unaudhofisha mwili kiafya hivyo kuchelewesha uponaji.
Sita, kuwa na mawasiliano ya karibu na wataalamu wa afya pamoja na wakufunzi wa michezo lengo ni kupata taarifa muhimu za tatizo lako na ushauri wa haraka pale unapoona viashiria au dalili zisizo za kawaida.
Virutubisho au viini lishe vinapatikana katika makundi saba ya vyakula ikiwamo protini, wanga, mafuta, mboga, matunda, vyakula vya nyuzi nyuzi na maji.
Wanga ni pamoja na ugali wali, viazi, ndizi na mihogo na vya mafuta ni kama vile mafuta ya mimea na wanyama. Vyote hivi hutupa nguvu na joto.