*Bado haijawa proved kwamba alijirusha mwenyewe, tunaendelea na upelelezi wakati tulipoenda kukagua eneo la tukio tulikuta pochi yake ikiwa na simu ambapo hatukuzikuta line zote mbili kwenye simu hiyo lakini pia simu moja na line yake havionekani kabisa, pili inasemekana aliwasiliana na mkurugenzi mkuu kwa njia ya E-mail kuwa akakabidhi document za ofisi ambazo bado zilikuwa mikononi mwake cha kushangaza documents zinakabidhiwa saa kumi usiku?, tumeenda kukagua cctv camera kuna baadhi ya matukio haonekani mfano ilifika sehemu Sr. anapanda ngazi mara ghafla akapotea mpaka tukashtuka nikiwa na Rco, kwa kweli ni mambo ya ajabu tulioyaona. Na ukumbuke pia kabla tulikuwa tunapeleleza upotevu wa zaidi ya Tshs. Milioni 500, ambapo yeye alikuwa mkuu wa idara ya fedha lakini katika uchunguzi wetu tuligundua watu wa chini yake ndio waliohusika kupiga hizo hela kwa kufungua akaunti tofauti na zile za hospitali. Lakini vilevile ikumbukwe BMC inamilikiwa na Kanisa katoliki na serikali pia hivyo kuna pande mbili za uongozi na inavyosemekana hizi pande mbili hazikuwa na maelewano mazuri. Kitendo cha Sister huyu kudondoka kutoka katika corridor ya ghorofa ya tatu karibu kabisa na dirisha la mkurugenzi mkuu ambaye yuko upande wa serikali pia imeleta maswali mengi ya kujiuliza. Hiyo ndio taarifa ambayo naweza kuwajulisha kwa sasa, tuacheni tufanye upelelezi then tutakuja na taarifa kamili*