Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

‪Mbunge Bobi Wine na Watuhumiwa wengine 30 wanatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Gulu nchini Uganda leo Agosti 30 kusomewa mashtaka yao kisha kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu kwani ndio yenye mamlaka ya kuendesha kesi ya uhaini inayomkabili Bobi Wine.
 
‪Kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) Julius Malema amewaambia Waandishi wa habari kuwa bara la Afrika linatakiwa lianze kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha kuu ya mawasiliano kwa madai ya kwamba lugha hiyo inazungumzwa sana barani Afrika.
 
‪Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amewasili leo nchini Kenya kwa ajili ya ziara ambayo imelenga kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya taifa lake na Mataifa ya Afrika ikiwemo Kenya katika kipindi ambacho wanakaribia kujitenga na Umoja wa Ulaya.
 
‪Polisi nchini Kenya imewakamata Wanafunzi wawili wa Sekondari na Mwanachuo mmoja kwa tuhuma za kumuua Mwalimu Manasse Ong’ole wa shule ya Sekondari Guu nchini humo baada ya Mwalimu huyo kukataa kuwanunulia pombe Wanafunzi hao.
 
‪Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amesema kuwa Mbunge Bobi Wine alivunjwa pua yake na Watesaji na ana majeraha kadhaa mwilini mwake, Besigye amesema hayo baada ya Bobi Wine kumuonesha majeraha aliyonayo alipokwenda kumtembelea hospitalini.
 
‪Rais Trump ameishutumu nchi ya China kuhujumu jitihada za Marekani na Korea Kaskazini katika kuharibu silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea, China nayo imeikosoa Marekani kwa kuilaumu kuhusu uhusiano wake na Korea Kaskazini.
 
Wanaijeria hawatakubali. Wanataka mojawapo kati ya lugha zao (Kiyoruba, Kihausa au Kiibo.

Wengine wanapendekeza kuwa twende kimaeneo: Afrika Kaskazini (Kiarabu), Afrika Magharibi (Kiyoruba), Afrika Kusini (Kizulu), Afrika Mashariki (Kiswahili)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…