Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kauli ya Rais Magufuli juu ya sakata la Makontena


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria sambamba na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi.
 
Kwa msingi huo, hakuna mtu yoyote mwenye mamlaka ya kukopa, kutoa dhamana na kupokea misaada kwa niaba ya Serikali bila mtu huyo kukasimiwa mamlaka hayo na Waziri wa Fedha kwa mujibu wa sheria hiyo" amesisitiza Rais Magufuli.
 
Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 30 Agosti, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, wakati akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa wilaya hiyo, ambapo amesisitiza kuwa viongozi wote wajenge utaratibu wa kusoma sheria na kujiepusha kutumiwa kwa maslahi ya watu binafsi.
 
Kauli hiyo imekuja leo baada ya siku chache zilizopita, viongozi wawili wa serikali ya Tanzania wamekuwa wakitupiana maneno hadharani. Viongozi hao ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
 
Hata hivyo, Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania imelishikia kidedea suala hilo na kumtaka mkuu huyo kulipigia kodi ya kiasi cha shilingi 1.2 bilioni, kwa madai kwamba, kontena hizo, ziko kwa jina la mtu binafsi na zimekaa bandarini kwa zaidi ya siku tisini.
 
BBC imefanya mazungumzo na mtaalamu wa masuala ya siasa Goodluck Ng'ongo, ambae anasema kila kitu ambacho kinachozua mjadala sheria yake ipo wazi.

"Waziri Mpango anasimamia sheria na kanuni na Mkuu wa Mkoa anaonekana kuweka siasa."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…