Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MCHAPO(WHISK): Hii ni aina ya mashine ya kuchanganya unga ukitumia mkono (sio ya umeme) muhimu kuchanganya mayai au unga lakini inachukua mda mwingi. Unaweza kuanzia kupika keki kwa kuchangannya mahitaji yako ukitumia mchapo, lakini kama unataka kupika keki za biashara utahitaji mashine za umeme kukurahisishia kazi!
 
MASHINE ZA KUCHANGANYA UNGA (ZA UMEME)/ELECTRIC MIXERs; Kama unataka kupika keki za biashara, nakuhusia upate mashine ya kuchanganya unga ya umeme kwani inarahisisha kazi sana na keki haikupigi chenga! Sio lazima kuwa nayo lakini kuwa nayo ni kama umeajiri mikono miwili zaidi jikoni! huku mashine inakufanyia kazi ww unafanya kazi nyengine!
 
Ziko aina nyingi na kila brand za mashine ina kazi yake kulingana na ukubwa, nguvu yake nk, Kwa hivyo kabla hujanunua mashine, jiulize unataka kuitumia kwa kazi gani, utaitumia mda gani, inachanganya unga kilo ngapi kwa mara moja, nk
 
MIIKO SPESHELI YA KEKI (SPATULAS): Miiko hii nayo pia inapatikana ya chuma au plastiki, na ukubwa tofauti pia. Hii muhimu kwa kutoa/kufuta mchanganyiko wote kwenye beseni kutia kwenye kibati cha kuoka nk. (sio utumie mikono au vidole vyako!!!) Pia inatumiwa kusawazisha juu ya keki kabla kuokwa.
Miiko hii muhimu pia utatumia kwenye kupambia keki.
 
BRUSHI ZA PASTRY (PASTRY BRUSH): Zinapatikana na kutofautiana kwa urefu, umbo nk. Muhimu vinatumika kwa kupaka ute wa mayai (egg wash) juu ya keki ,au labda unapaka jam juu ya keki katika upishi wake au upambaji wake, nk.
 
VYOMBO/VIFAA/TREYA ZA KUOKA : Hizi nazo zinapatikana shepu na ukubwa tofauti na utapata viloundwa kwa chuma, glass, plastiki ya silicone, nk,
Muhimu utumie ukubwa au shepu ambayo recipe imekuhusia utumie au sivyo itabidi urekebishe mda wa kuoka!
 
OVEN/MOTO WA KUOKEA KEKI: Oven nalo muhimu kwa mapishi ya keki hasa kama unataka kuunda keki za biashara. Lakini nasisitiza sio lazima!. Kama huna oven, unaweza kupambia keki kwenye sufuria kutumia mkaa/makaa. Lakini kwa urahisi wa mapishi oven ni muhimu. Ikiwa huna unaweza kuanza biashara yako ukitumia moto wa mkaa/makaa lakini ujipange ununue oven la biashara ukifanikiwa kiuchumi.
Kumbuka nayo ma oven pia yapo tofauti tofauti. Muhimu ambayo yapo kwa wingi ni:
 
CONVECTIONAL OVENS (pia zinaitwa THERMAL au RADIANT OVEN):
oven hizi zinakuwa na wire ambazo utaziona zimeshika moto sehemu ya juu (zikiwa moto zinakuwa nyekundu) Oven hizi zinapika chakula kwa kusukuma upepo wa baridi kuelekea chini ya oven pindi sehemu ya juu inakuwa moto. Kwa hivyo huo upepo unaoshuka chini unaweza kufanya keki yako isiive uzuri au ikupige chenga,
Kama unalo oven, liangalie ndani ujue una oven aina gani ndio ulifahamu oven lako!

>> CONVENTION OVEN: Oven hizi zinakuwa na kifaa cha kupuliza upepo (fan)(ambacho kawaida kinakuwa ndani lakini nyuma mwa oven lako). Upepo wa joto unapulizwa mwote ndani ya oven kwa hivyo keki inaiva haraka na kwa uzuri sana. Kwa ajili hiyo, mda wa mapishi kawaida unakuwa mfupi kulinganisha na oven lilotajwa hapo juu la convectional oven.
 
KWA HIVYO LITAMBUE OVEN LAKO!! Unaweza kupika keki ukafuata maagizo yote lakini ukaona imeungua kwenye kuokwa japo umeoka kwa mda ulopewa wa recipe. Basi ujue labda oven unalotumia ni 'convection oven' kwa hivyo mda ulifaa uupunguze kidogo! Nadhani hapo umeelewa? Lifahamu oven lako!

ANGAZO: Kumbuka hata maoven ya brand moja pia yanatofautiana, muhimu ni ulijue oven lako binafsi kwa kulifanyia mazoezi mpaka uliewe ndio utajua wapi unakosea kwenye upishi wa keki.
 
SAA YA JIKONI KWA UPISHI (KITCHEN TIMER) : Kuna oven nyengiine nazo zinakuwa na kifaa cha kuhesabu na kubainisha mda (digital timers) lakini ukiwa na saa ya jikoni utakuwa unapima mda sahih unaotakikana kwani saa nyengine za oven huwa zinapoteza mda au kuharibika! Na kama nilivyosema awali, upishi wa keki unataka makini, ukiambia oka kwa mda wa nusu saa basi ukizidisha keki itakuwa ngumu. Keki la upishi halitaki kukisiwa!

10: KIFAA CHA KUPOZA KEKI (COOLING RACK): Baada ya kuoka keki, inafaa ipoe kidogo kisha unaitoa kwenye chombo ulichookea unaiweka kwenye hichi kifaa ili ipoe moto kabisa bila kufanya mvuke. Hii muhimu sana kwa keki ambazo ungependa kuzipambia kwa fondant baadae..

UKIWA NA VIFAA HIVI (JAPO) VICHACHE VILOTAJWA HUMU, UPO TAYARI KWA UPISHI WA KEKI WA KUJIANDALIA BINAFSI AU KWA MADHUMUNI YA BIASHARA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…