Wanaume wa Dar. Ujumbe wenu huu
**************************
DAR YA PILI KWA WATU WAOGA ZAIDI AFRIKA.
Mtandao wa citypages.com umelitaja jiji la Dar es Salaam kama jiji la pili kwa watu waoga zaidi Afrika (Cities with the most coward people in Africa). Utafiti uliofanywa na mtandao huo unaonesha kwamba wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam ni waoga hata katika mambo ambayo hawakupaswa kuogopa.
Utafiti huo ulifanywa kwa kuhoji mambo anuai yaliyohusu ujasiri wa watu katika miji ya Afrika, hususani miji mikuu au miji mikubwa ya Kibiashara ya nchi za Afrika.
Jiji la Cairo limeshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na watu wenye ujasiri zaidi, likifuatiwa na jiji la Mogadishu nchini Somalia. Jiji la Dar es Salaam limeshika nafasi ya pili kwa kuwa na watu waoga zaidi Afrika likitanguliwa na jiji la Lusaka nchini Zambia.
Mmoja kati ya watu waliotoa maoni yao katika utafiti huo amesema "Dar es Salaam is the place that you can intimidate someone and get applause if expose a weapon" akimaamisha jiji la Dar ni mahali ambapo unaweza kumuonea mtu akakutukana moyoni lakini ukimuonesha silaha akakupongeza kwa kumuonea."
Orodha kamili ya miji yenye watu waoga zaidi Afrika ni:
1. Lusaka (Zambia)
2. Dar es Salaam (Tanzania)
3. Blantyre (Malawi)
4. Mombasa (Kenya)
5. Banjul (Gambia)
6. Mbabane (Swaziland)
7. Gaborone (Botswana)
8. Cotonou (Benin)
9. Victoria (Seychelles)
10. Rabat (Moroco).