Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa mara ya kwanza katika miaka 10, mshambuliaji Lionel Messi ameshindwa kuingia katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa, huku Cristiano Ronaldo, Mo Salah na Luka Modric wakiingia katika kinyang’iro hicho.

Nyota huyo wa Barcelona msimu uliopita alifunga mabao 44, pamoja na kutwaa taji la La Liga na Kombe la Mfalme.
 
Messi na Argentina waliondolewa katika hatua 16 bora katika Kombe la Dunia iliyochukuliwa na Ufaransa kwa mara ya kwanza katika miaka 11 ameshindwa kuingia katika tatu bora.

Wakati Messi akiondolewa mshindani wake mkubwa katika miaka 10 iliyopita wakipokezana mara tano kila mmoja Ronaldo ameingia katika tatu bora.
 
Ronaldo, Luka Modric na Mohamed Salah, wameingia katika orodha hiyo kama ilivyokuwa katika tuzo za mwanasoka bora wa Ulaya iliyotwaliwa na Modric.

Wachezaji hao watatu walikuwa na mchango mkubwa kwa klabu zao pamoja na timu zao taifa katika Kombe la Dunia mwaka huu.

Tuzo ya mchezaji bora wa 'FIFA Ballon d'Or,'' inapatikana kwa wachezaji kupigiwa kura na manahodha wa timu za taifa, makocha na wanahabari pamoja mashabiki kupitia tovuti ya Fifa.
 
Wanaowania tuzo hizo

Mchezaji bora kwa wanaume: Cristiano Ronaldo, Luka Modric, Mo Salah

Tuzo ya Wanawake- Ada Hegeberg, Dzsenifer Maroszan, Marta

Tuzo ya Shabiki bora wa FIFA- Sebastian Carrera, mashabiki wa Japan na Senegal, Peru.

Kocha bora wanawake - Reynald Pedros, Asako Takakura, Sarina Wiegman

Kocha bora wanaume- Zlatko Dalic, Zinedine Zidane, Didier Deschamps

Tuzo ya Puskas - Gareth Bale, Denis Cheryshev, Lazaros Christodoulopoulos, Cristiano Ronaldo, Giorgian De Arrascaeta, Riley McGree, Lionel Messi, Benjamin Pavard, Ricardo Quaresma, Mo Salah
 
Kipa bora- Thibaut Courtois, Hugo Lloris, Kasper Schmeichel

Nyota waliowahi kushindi tuzo hiyo:-

5: Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.-

3: Ronaldo Nazario, Marco van Basten na Zinedine Zidane.-

2: Ronaldinho na Lothar Matthaus.-

1: Roberto Baggio, Romario, George Weah, Rivaldo, Luis Figo, Fabio Cannavaro na Kaka.
 
  1. luka modric
  2. muhammed salah
  3. cristiano ronaldo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…