Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amepiga marufuku wabunge wanawake wenye kucha na kope za kubandika wasiingie bungeni.

"Kwa mamlaka niliyopewa, napiga marufuku wabunge waliobandika kucha za bandia na kope za bandia kwamba ni marufuku na hilo la kujipodoa bado najadiliana na wataalam wangu," amesema Spika.

Spika Ndugai alitoa kauli hiyo leo bungeni muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa afya, Dk Faustin Ndugulile kutoa majibu ya madhara makubwa wanayopata wanawake wanaotumia kucha na kope za bandia.
 
Naibu Waziri alisema takribani wagonjwa 700 hupokelewa kwa mwaka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa na matatizo ya ngozi yatokanayo na kumeza vidonge vinavyobadili sura pamoja na vipodozi vyenye kemikali na kuwa watu hao wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya saratani na ya ngozi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Fatuma Toufiq alihoji ni wanawake wangapi wameathirika macho kutokana na matumizi ya kope bandia.
 
Naibu Waziri alisema kucha na kope za kubandika si vipodozi kwa mujibu wa sheria ya chakula, dawa na vipodozi sura ya 219 inayosimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

"Kwa mujibu wa sheria hiyo, kipodozi ni kitu chochote kinachotumika kwenye mwili au sehemu ya mwili," alisema Dk Ndugulile.
 
Naibu Waziri alisema kucha na kope za kubandika si vipodozi kwa mujibu wa sheria ya chakula, dawa na vipodozi sura ya 219 inayosimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

"Kwa mujibu wa sheria hiyo, kipodozi ni kitu chochote kinachotumika kwenye mwili au sehemu ya mwili," alisema Dk Ndugulile.
 
Serikali ina mpango wa kuajiri watendaji kata 1,000 ili kupunguza pengo kubwa la ukosefu wa watendaji hao katika maeneo mengi nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kandege.

Kandege alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tundulu Kusini (CCM), Daim Mpakate ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itaajiri watendaji kata kwani maeneo mengi yako wazi.

Naibu Waziri huyo alikiri watendaji ni watu muhimu katika shughuli za maendeleo hivyo Serikali imeona umuhimu wa kuwaajiri ili kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.
 
Tumeomba kibali na tumepewa kuajiri watendaji kata 1,000, hivyo tuna amini tukishaajiri hao tutakuwa tumepunguza pengo hilo kwa kiasi kikubwa," alisema Kandege.

Naibu Waziri huyo alisema mpango huo utafanyika mapema kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa.

Kuhusu posho za wenyeviti wa serikali za mitaa alisema kila halmashauri imekuwa ikisisitizwa kurudisha asilimia 20 ya mapato yake kwenye maeneo husika ili zisaidie kulipa posho za viongozi hao.
 
Jeshi la Polisi jijini hapa limesema watu saba wamejeruhiwa, huku wanne kati yao wakiwa mahututi baada ya kushambuliwa na mwanaume mmoja aliyekuwa na kisu.
Watu waliokuwa karibu na tukio hilo waliokuwa wanacheza mchezo wa kulenga mipira ya chuma maarufu kama 'petanque' walijaribu kumdhibiti mshambuliaji kwa kumrushia mipira hiyo.
Hata hivyo, mshambuliaji huyo aliyetambulika kuwa ni raia wa Afghanistan alikamatwa muda mfupi baadaye, ingawa maofisa wa polisi hawajalichukulia shambulio hilo kuwa la kigaidi.
 
Back
Top Bottom