Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mshukiwa alianza kuwashambulia wanaume wawili na mwanamke mmoja karibu na ukumbi wa sinema wa MK2 katika mtaa wa Quai de Loire pembezoni mwa mfereji wa Ourcq, baadhi ya ripoti zinasema.
Shuhuda Youssef Naja (28) alisema alikuwa anatembea kando ya mfereji alipomwona mshambuliaji akikimbia akiwa ameshika kisu chenye urefu wa takriban inchi kati ya 10 na 11.
“Kulikuwa na watu kama 20 waliokuwa wanamkimbiza. Walianza kumrushia petanque. Mipira takriban mitano ilimpata lakini haikusaidia kumwangusha,” alisema.
 
Baadaye iliripotiwa pia kwamba mshambuliaji huyo aliwashambulia watalii raia wa Uingereza katika mtaa jirani kabla ya kukamatwa.
Ofisi ya masuala ya kigeni ya Uingereza imesema kwamba inalichunguza suala hilo kwa ukaribu. “Tunalifuatilia tukio hili kwa ukaribu sana na mawasiliano ya karibu na mamlaka za Ufaransa,” alisema.
Idara ya polisi ya Ufaransa imesema hakuna viashiria vyovyote vya ugaidi katika tukio hilo mpaka sasa. Kwa kipindi cha miezi michache iliyopita kumekuwa na mashambulizi kadhaa ya visu nchini Ufaransa huku machache yakihusishwa na mashambulizi ya kigaidi. (BBC)
 
Kope na kucha si mnabandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…