Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Jorge Mas, aliwasihi mashabiki wote wa soka wa mji wa Miami kuiunga mkono kwa dhati timu hiyo ya nyumbani akisema wanatarajia itakuwa moja ya timu kubwa za soka nchini Marekani.

Alisema wanajivunia mapenzi ya wana Miami wote na kwamba wameridhishwa na mapokezi ya timu hiyo wanaamini wataiunga mkono na kuifanya kuwa moja ya timu kubwa za soka duniani miaka michache ijayo.
 
Hatimaye timu ya Taifa ya England, imemaliza jinamizi lililoiandama la vipigo vitatu mfululizo baada ya jana Marcus Rashford kuifungia bao pekee ilipoilaza Uswisi 1-0, katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Ushindi katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa King Power wa timu ya Leicester City, umemwezesha Kocha wa England, Gareth Southgate kupumua baada ya kujiondoa kwenye kipindi kigumu cha matokeo ya kuumiza.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 England ilijikuta ikipoteza mechi tatu mfululizo baada ya kufungwa na Croatia mabao 2-1 katika nusu fainali ya Kombe la Dunia na baadaye kufungwa na Ubelgiji 2-0 katika mechi ya kusaka nafasi ya tatu kabla ya kufungwa 1-0 na Hispania katika mechi ya mashindano ya β€˜Euro Nations League’.
 
Mshambuliaji chipukizi asiye na uhakika wa namba katika timu yake ya Manchester United, Marcus Rashford ndiye aliyeifungia nchi yake bao hilo muhimu katika dakika ya 54 akiunganisha krosi ya mlinzi Kyle Walker.

Kocha Southgate atafurahia uamuzi wake wa kutumia washambuliaji wawili mbele ambapo Rashford alishirikiana na Danny Welbeck huku nyuma yao kukiwa na viungo watano jambo lililomaanisha kuwa walipania kucheza kwa kujilinda licha ya kuwa nyumbani.

Kiungo nyota wa Uswisi, Xherdan Shaqiri alikaribia kuwafunga wenyeji mara mbili katika kipindi cha kwanza ambapo shuti lake la hatari zaidi liligonga mwamba kabla ya kuokolewa.
 
Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone amesema hana mpango wa kumsajili mwanae wa kumzaa Giovanni Simeone, licha ya kuwa na kiwango bora kwa sasa.

Simeone alimmwagia sifa mwane huyo mwenye miaka 23 ambaye ni mshambuliaji akisema kwa sasa amekamilika kiuchezaji, ingawa yeye hana mpango naye.

β€œKwa hakika hivi sasa Giovanni anacheza soka la uhakika nimekuwa nikimfuatilia katika timu yake ya Fiorentina aliyojiunga nayo akitokea Genoa pia ya Italia mwaka jana,” alisema.
 
Aliongeza kuwa wakati akitua Genoa akitokea River Plate ya Argentina Agosti 2016, alikuwa anahitaji kujifunza mambo mengi ili kuwa mchezaji bora lakini kwa sasa amekamilika na anaweza kucheza kwenye klabu yoyote ile.

Giovanni aliifungia Genoa mabao 13 msimu uliopita na kuishawishi Fiorentina kutoa Euro 18 milioni Agosti 2017 na akalipa fadhila kwa kufunga mabao 15 katika mechi 41 alizoitumikia msimu uliopita.

Alisema anachotamani kwa sasa kukiona kwa mwanae ni kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina lakini sio kumsajili ili aitumikie Atletico kwa kuwa kufanya hivyo kutawapa wote wawili mazingira magumu ya ufanyaji kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…