Ukiona mtu analalamika, analalamikia serikali, wazazi, ndugu, marafiki na kujilalamikia mwenyewe, Muda wake umekufa, hafikiri na yupo gizani. ana macho lakini haoni furusa, ana masikio lakini hasikii . Hana mafunuo . Hayupo na Mungu.
Siku ukiona fursa umeona maisha.Watu wanaweza wakakudharau lakini kumbe ulichonacho ndani yako ni kikubwa. umebeba mafunuo makubwa.
Kwa hio usilegee, bali ijapokuwa utu wako wa nje umechakaa, lakini utu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio.
Tusiangalie vinavyoonekana bali visivyooonekana, kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu, bali visivyoonekana ni vya kudumu.
Usikubali mtu akudharau, wewe una akili , wewe ni wa kipekee, wewe ni shujaa, Jitambue upesi.
Mungu atakutengeneza na kukuthibitisha na kukutia nguvu.
Tafuta kupata mafunuo ya Mungu.