Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6adf166c-6f41-42ac-a88b-b3ec22c99aae~2.jpeg
 
Kujijali ni kitu gani? ni hali ambayo inahitaji kupata muda wa kutulia ukiwa mwenyewe kwa ajili yako na maendeleo ya maisha yako badala ya kusubiri mtu mwingine kukujali wewe.

Mara nyingi watu wanauliza unawezaje kujijali ukiwa na majukumu ya kuhudumia wengine ? Jibu ni kwamba , huo ni mtazamo wa mtu . Lakini kama utafahamu kutumia muda wako vizuri unaweza kuchukua nafasi kwa ajili yako. Unatafuta muda katikati ya muda wako kutulia kila siku kwa dakika kadhaa mahali ambapo pana utulivu ili kuongeza nguvu mpya, mawazo mapya . Utatumia muda wako kwa kukaa tu bila ya kufanya kitu , ukiwa umetulia .

Ukiwa unafanya hivyo kila siku , hautakuwa na stress za aina yoyote , bali utaishi maisha bora.
 
Hapa chini kuna njia 10 za kufanyia mazoezi ya kukufanya ujijali.

1.Kujijali maana yake ni kujitambua wewe ni nani na una mipaka gani

Ni kutambua wakati unapokuwa umezidisha kitu katika majukumu yako . umepitiliza kiwango cha kile unachotakiwa kufanya. Ni kuelewa namna ya kurekebisha yote ambayo yanakutatiza.
 
2.Kujijali maana yake ni jinsi unavyojiona mwenyewe.

Kujua matumizi ya muda, kufafamu muda wako wa kupumzika na wa kulala na muda wako wa kufanya kazi , Kufahamu ratiba yako ya kila siku, ya wiki, ya mwaka. Na kufahamu jinsi ya kutunza mwili wako , Akili yako na Roho yako. kujipenda, kujithamini, kujiona mshindi kuanzia ndani mwako.
 
3.Kujijali ni Kumpenda Mungu, Kuwapenda watu na kuipenda nafsi yako.

Chochote unachopenda ufanyiwe wewe, jaribu kuwafanyia wengine. Ukimpenda Mungu kwa nguvu zako zote, akili yako yote, moyo wako wote na roho yako yote, na kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Kuacha kula vitu ambavyo sio salama kwa afya yako. kuacha dhambi ili kuondokana na hofu , mashaka mbalimbali kwenye maisha yako.
 
Back
Top Bottom