Watu ambao wanasubiri kufanya kitu baadae , hawajijali na wala hawajitambui. Una masaa 24 kila siku kwa nini usitumie muda wako kufikiri mambo yaliopo wakati huo. Utakuta mtu ana kitu cha kufanya lakini anasema nitafanya kesho, wakati uwezo wa kufanya hicho kitu anao. Unapoteza muda mwingi sana . Utashindwa kujijali mwenyewe. Kama huna Nidhamu ya mitandao huwezi kuishi wakati uliopo. kama hutumikishi mwili wako sawasawa hutaweza kuishi wakati uliopo. Watu wengi wanaugua magonjwa ya kutofanya kazi za kutosha.
Kama huna kazi za kutosha nitafute nikufahamishe kazi za siku nzima, ambazo zitakufanya ujione nawe unaishi.
5.Kujijali maana yake ni kutoa wazo ambalo litatatua Hali ngumu ya kazi uliyonayo.
Tunafahamu ni kitu gani tunahitaji na nini cha kushughulikia. Kipo kitu ambacho kinaweza kufanya kazi yako iwe rahisi, njia hio ni kufanya kitu unachokipenda. Mahali ambapo utajisikia vizuri kila unapokuwepo kazini kwako, masaa unayotumia kazini kwako, muda wa kujisomea , muda wa kula na muda ambao sio wa kula. Unajitawala mwenyewe. Wewe ndiye mkurugenzi wa maisha yako, na ni Raisi wa muda wako.
6.Kujijali maana yake ni kupata muda wa kujifahamu vizuri.
Kujiwekea mipaka yako, kutambua wakati umezidiwa na kitu na kukirekebisha haraka , Kutambua hisia mbaya na nzuri zinazojitokeza kwako na kama ni mbaya unakabiliana nazo mara moja. Kumsikiliza Mungu zaidi kuliko kusikiliza watu.
7.Kujijali maana yake ni kujua kitu kinachokufurahisha na kitu ambacho kinakutoa kwenye hali ya amani.
Kuzitambua hisia ambazo sio zako na kuziondoa , kutengeneza tabia nzuri kila siku kwa kusoma Neno la Mungu zaidi na kujitahidi kuhudhuria semina mbalimbali. Jaribu kuwa na mtu wa karibu ambaye kila ukimpigia simu unafurahi kuongea naye. usiende sehemu ambayo itakukosesha amani
8.Kujijali maana yake ni kutopitia mahali ambako hukupanga kupitia .
Unaweza ukawa unarudi nyumbani ukitokea kazini , ukakutana na mtu akaanza kukushawishi kwenda Bar. kama hukupanga usiende. huenda akakuambia mwende sinema lakini hukupanga, usiende.
9.Kujijali Maana Yake ni Kulisha nafsi yako kitu kizuri.
Hii ni pamoja na kufanya tafakari, kuomba, kutembea kwa muda wa dakika 30, kuhudhuria ibada, semina. kuwa mtu wa shukurani, kusoma na kusikiliza kitu ,