Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Neymar anatazamiwa kupokelewa kwa chuki na mashabiki wa Liverpool ikiwezekana pamoja na wachezaji wa timu hiyo baada ya hivi karibuni kudai Liverpool haina nafasi ya kuwepo katika timu nne bora mwishoni mwa msimu huu.

“Nani atashinda? Ah itakuwa ngumu sana. Ni ngumu sana, ngumu sana lakini Manchester City itashinda ya pili itakuwa Manchester United, ya tatu itakuwa Chelsea na ya nne itakuwa Tottenham,” alisema Neymar mapema mwezi huu akiipuuza Liverpool

Mashabiki wa Liverpool wameonekana kufurahishwa na uteuzi wa Mwamuzi Cakir kutokana na rekodi maarufu aliyonayo mwamuzi huyo wa Uturuki kwao. Mechi pekee aliyochezesha kwao ni katika ushindi dhidi ya Borussia Dortmund michuano ya Europa msimu wa 2015/16. Katika pambano hilo kocha wa Dortmund alikuwa Tuchel ambaye kwa sasa amehamia PSG.
 
Rekodi ya Cakir kwa mechi za PSG pia itawafurahisha mashabiki wa Liverpool baada ya rekodi kuonyesha katika mechi mbili ambazo ameisimamia timu hiyo ya Paris zote walishindwa kupata matokeo.

Mechi ya kwanza ilikuwa ni hatua ya makundi dhidi ya Chelsea mwaka 2015 ambapo pambano lilimalizika kwa sare ya 1-1. Vilevile alisimamia mechi ya makundi ambayo walichapwa mabao 3-1 msimu uliopita.

Katika pambano la leo, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anatazamiwa kumpanga staa wake wa kimataifa wa Brazil, Roberto Firmino ambaye alipelekwa hospitali na kulazwa baada ya kuumizwa jicho na beki wa Tottenham, Jan Vertonghen katika pambano dhidi ya Spurs Jumamosi.
 
Kwa upande wa PSG, Kocha Tuchel anatazamiwa kumchezesha staa wake wa kimataifa wa Ufaransa, Kylian Mbappe ambaye kwao amefungiwa mechi tatu za michuano ya ndani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu hivi karibuni kwa kumpiga mchezaji wa timu pinzani.
 
STRAIKA wa Tottenham Hotspur, Harry Kane hataki kukubali kuwa uchovu unamfanya apoteze makali yake ya kufunga mabao baada ya kutoka kapa kwenye mechi dhidi ya Liverpool Jumamosi.

Kumekuwa na maneno Kane ametumika sana kuanzia msimu uliopita hadi kwenye Kombe la Dunia 2018, mahali ambako alifunga mabao mengi yaliyomfanya ashinde Kiatu cha Dhahabu cha michuano hiyo iliyofanyika huko Russia, lakini tangu aliporudi kwenye ligi msimu huu, hana tena maajabu.

Fowadi huyo amewashangaza wengi baada ya kucheza kwa dakika 249 sasa bila ya kufunga bao lolote, lakini mwenyewe anaamini atarudi kwenye makali yake na hilo litaanzia leo Jumanne huko San Siro ugenini kwa Inter Milan, ambao ataikabili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Watu siku zote wamekuwa wakitafuta sababu tu, hasa ukiwa mchezaji muhimu kwenye timu na mfungaji wa mabao. Tukiwa kama timu, sote tunapaswa kufanya vizuri,” alisema Kane na kuongeza: “Kocha ndiye mwenye uamuzi wa mwisho. Ananiamini na najiamini pia, hivyo naamini nitafunga mabao Jumanne na kuzima hizo kelele zote.”

Kane ameifungia Spurs mabao mawili tu katika mechi tano za mwanzo wa msimu huu walizocheza kwenye Ligi Kuu England.
 
Kiungo mahiri wa Chelsea, Ng’olo Kante, amesema kuwa alipokea ofa nyingi za kuondoka kwenye klabu hiyo mara baada ya kumalizika kwa Fainali ya Kombe la Dunia 2018, ikiwemo ya mshahara mnono kutoka PSG.

Kante ambaye alisaidia kuipa Ufaransa taji hilo la pili katika historia ya Taifa hilo, alisema pamoja na ahadi nyingi aliamua kubakia Stamford Bridge.

Mchezo huyo alitwaa taji la Ligi Kuu England kwa misimu miwili mfululizo alitwaa msimu wa 2015/16 akiwa na Leicester City na msimu uliofuata akatwaa tena akiwa na Chelsea.

Alisema yeye mwenyewe hakujua mustakabali wake ndani ya Chelsea kabla ya kuanza kwa msimu huu hadi alipokaa na kocha mpya Maurizio Sarri, ambaye baada ya mazungumzo ya kina alimuhakikishia namba na kumpa uhuru wa kucheza.

"Baada ya kuzungumza na Kocha Sarri, niliamua kubakia Chelsea, kuna mambo mengi tulijadili ya msingi, aliponiambia kuwa atatuhusu wachezaji wote kucheza tuwezavyo kwa uhuru nilijua wachezaji wengi watabaki kwa sababu tangu enzi za Antonio Conte, wachezaji walikuwa wakililia kucheza kwa uhuru,” alisema.

Alisema hata Eden Hazard aliyetaka kwenda Real Madrid na Alvaro Morota walitaka kuondoka Chelsea, kwa sababu Conte aliwanyima uhuru wa kucheza soka uwanjani, jambo ambalo huwafanya wachezaji kutofanya vizuri na kujikuta wakibeba lawama za timu.
 
naye kaamua kumkuza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…