Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadharisha kutokea mvua kubwa ndani ya siku tatu kuanzia kesho hadi Alhamisi Septemba 27, 2018,.

Kutokana na utabiri huo, TMA imewataka wananchi kuchukua tahadhari.

Taarifa ya mamlaka hiyo, iliyotolewa leo jioni Septemba 25,2018 imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni Tanga, Dar es Salaam, Pwani pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.

Taarifa hiyo imewataka wananchi wa maeneo husika kuchukua tahadhari kwa sababu mvua hizo ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 70.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…