Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pambano Watani wa Jadi Simba na Yanga lilimalizika kwa suluhu sasa yamebaki maneno kwa mashabiki wao ambao kila kona ya kitaa wanatambiana kwa ubora.

Mbali na kelele hizo za mashabiki ndani ya dakika 90 za mchezo kuna mambo mengi yalijitokeza.
 
1. KAKOLANYA KUSHANGAZA WATU

Katika mechi hiyo kama si ubora wa kipa, Benno Kakolanya wa Yanga kuokoa michomo ya wazi ya wachezaji wa Simba basi watoto hao wa Jangwani wangeumia.

Kakolanya alikuwa katika kiwango bora akafanya awe gumzo kwa mashabiki wote wa soka nchini si Simba wala Yanga na kumdhihirishia kocha wake mkuu, Mwinyi Zahera aendelee kumwamini.
 
2. SIMBA UTULIVU

Katika mchezo huo, Simba watajilaumu kutokana na wachezaji wao kukosa utulivu haswa katika sehemu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Mnyarwanda Meddie Kagere na Emmanuel Okwi ambao walikosa

mabao ya wazi.

Wachezaji wa Simba wangekuwa watulivu na makini katika mechi hiyo wangeifanya timu hiyo iibuke na ushindi kwani walipata nafasi za kufunga zaidi ya tano lakini walishindwa.
 
3. MAAGIZO YA AJIBU

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu alikuwa gumzo katika mechi hiyo mara baada ya kuanza mpira kwa kuupiga nje badala ya kucheza jambo lililowashtua baadhi ya wapenzi na mashabiki wa soka wakiamini ni imani za kishirikina.

Lakini, huenda likawa jambo la kawaida tu katika soka au Yanga walitaka kuwachezea akili Simba. Klabu ya Marseille ya Ufaransa walishafanya hivyo dhidi ya Atletico Madrid ya Spain.
 
4. YANGA KUPAKI BASI

Katika mechi hiyo, Yanga waliingia wakizuia tu na si kushambulia kwani kikosi chao kilianza na mfumo wa mabeki watano, viungo wanne na mshambuliaji mmoja, (5-4-1) jambo ambalo mpaka mechi inakwisha ilikuwa suluhu.

Kwa upande wa Yanga walifanikiwa kutokana na aina yao ya uchezaji waliyotaka kucheza.

Simba walimiliki mpira muda mwingi kuliko Yanga lakini walikaa nyuma ya mpira na kucheza kwa kujilinda zaidi na hata mechi ilipomalizika kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alikubali hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…