DARASA HURU.
WEWE MWENYEWE MWENYEWE NDIYE RAFIKI
WA KWELI KATIKA MAISHA YAKO
Hakuna atakayekupenda kama wewe, hakuna
atakayekuheshimu Kama wewe, hakuna atakaye
kutunzia siri zako kama wewe, hakuna
atakayekuthamini kama wewe, hakuna
atakayefurahia mafanikio yako kama wewe,
hakuna atakayekuhurumia Kama wewe.
Jifunze kujifurahia, kujipenda, kujisahihisha
unapokosea, jifunze ku-enjoy company yako
mwenyewe, Jifunze kumtafuta Mungu
mwenyewe kwa bidii bila kulazimishwa maana
Yeye ni uzima na afya mifupani mwako...
Jifunze kujiwekea mipaka itakayokufanya
uheshimike, usiongee kila kitu( kuwa na mipaka
kwenye kinywa chako)
Shibisha akili yako na vitabu vinavyojenga, kula
chakula chenye afya, jitengenezee mazingira
rafiki hasa kwenye nafsi yako, jisemee mambo
mazuri, jishughulishe ili usiwe tegemezi.
Mara moja moja ukipata nafasi jipe likizo.
Ukianguka amka, jikung'ute mavumbi, na songa
mbele.
Ukihisi kuumizwa na kusalitiwa kwa namna
yoyote ile;lia kidogo, futa machozi kisha songa
mbele. Usipoteze muda wako kukaa katika
maumivu kwani siku zako za kuishi
zimehesabiwa.
Usikubali maneno mabaya ya walimwengu
yajenge kiota kwenye kichwa chako.
Usikubali mtu akuumize bila ruhusa yako.Jifunze
kuondokana mazingira au makundi unapoona
yanakuondolea amani na kudhoofisha afya ya
nafsi yako.
Jifunze kuridhika na ulichonacho huku
ukipambana kuwa bora kuliko jana.
Usipende kujilinganisha na wengine hasa kwenye
mafanikio labda ukiwa na lengo la kujifunza tu ili
na wewe uongeze bidii na juhudi za kufanikiwa...
Mwisho kabla ya kujenga urafiki na wanadamu,
jenga urafiki wa karibu na Mungu wako anayejua
mwanzo na mwisho wa maisha yako.
Otherwise FURAHIA UHAI ULIOPEWA NA MUNGU
NA UTENDEE HAKI UZIMA WAKO