Jamii ibadilike sasa, ifuatilie nyendo za watoto bila kujali ni wa familia ya nani, kwa sababu hakuna aliye salama tena, ” alisema.
“Huu siyo wakati wa kuwaacha watoto wacheze kiholela, kwa sababu hakuna umri maalumu wa watoto kupotea, wanawachukua wenye umri mdogo.”
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa alisema wazazi wana jukumu la kuhakikisha watoto wao wanapokuwa mahali popote wana ulinzi kamili ili wasiingie kwenye mikono ya wahalifu.
“Kwa mfano kuna mtu anacheza na mtoto wako humjui au unamfahamu juujuu, upo na unaangalia, siku akija na kutaka kuondoka naye mtoto hatakataa atakubali akipotea ndiyo inabainika kuwa licha ya kumuona akicheza na mwanao kila siku hufahamu vizuri anaishi wapi,” alisema Mwakalukwa.