Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanamwali

Nilimwona akinijia
Katika ukungu wa fikra kavu
Na manyunyu ya upendo wenye madoa
Katika asubuhi ile nyekundu
Mwendo wake ulikuwa wa tahadhari sana
Alionekana kama anatembea juu ya mayai
Au mawingu mazito yenye matobo
Akija na kwenda kama hanijui
Kwa nini bado hajafika?
Ni kweli yungali akija?
Wanauzi mkionana naye mwambieni...
Bado namsubiri........


-SYB (JF)
7/10/2018
 
[emoji848]
 
Na kwa jinsi ulivyo kazia msisitizo wa asante...tutabarikiwa ..vyema....sana.

Ameen ..
 
Kubariki ni kazi ya Mungu; na Yeye huwa haangalii msisitizo wa maneno bali wa kimatendo tena uliosimikwa katika imani thabiti !!!
Kubariki ni kazi ya Mungu ni kweli na sisi tumeomba na kuitikia kupitia mkuu sweetlee ... msisitizo ni muhimu ndio imani thabiti onekanavyo.. vitendo ni kuomba na kuitikia.. .
. .. haya ..nakazia ..

Amen..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…