Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Iyo conclusion duh yaani inahuzunisha kwa kweli.yaani jitihada za kumftafuta akiwa hai zilishindikana ama vipi[emoji853][emoji853][emoji853][emoji853]
Kwenye upelelezi kama huu unafuata credible info zinakokupeleka. Kama umesikia kuwa katupwa majini huwezi kwenda porini inabidi uende huko huko majini. Na habari hizo zinaweza kuwa kweli ama la kwa sababu katika kesi kama hizi unapata habari za kila aina.
 
Umesema vyema.. Ila tunapokua haturidhiki katika chunguzi kulingana na matukio na kuonekana viashiria vya upendeleo unategemea sisi wananchi tuseme nini?
 

Issue ni mipango wa kusearch,

Yani ukitafakari mkakati unaotumika kumtafuta MO unaona kabisa Polisi haina nia ya dhati, na hii inaumiza zaidi.

Tuna laumu hatuna vitendea kazi lakin ukweli ni kwamba tunavyo na tunaamua kutovitumia kwa sababu tusizozijua.

Mf. mzuri ni kwa MV Nyerere, PM alifika na chopa cha kushangaza giza lilivyo ingia walishindwa kutumia chopa kama source ya mwanga kuendelea kuokoa watu.

Swala la MO, Asbh ile ndo ulikuwa muda wa kutafuta baharini iwe ni boat ama chopa. Sasa a day after unategemea nini.?
 
Umesema vyema.. Ila tunapokua haturidhiki katika chunguzi kulingana na matukio na kuonekana viashiria vya upendeleo unategemea sisi wananchi tuseme nini?
Kuna viashiria gani vya upendeleo kwenye hii kesi, kwa mfano? Huyu ni mtu tajiri kuliko wote hapa nchini na mambo yako hivi, unafikiri angekuwa mtu baki tu kama mimi (na pengine wewe) hali ingekuwaje? Tuna mifumo mibaya ya kiintelijensia, kiusalama, kipolisi, kitabibu, kiusafirishaji, kisiasa...you name it. Na chanzo cha yote ni likatiba libovu lililopitwa na wakati, katiba ambalo linaendekeza sheria zisizo na meno na zinazokuza tabia za kulindana, ufisadi, kuoneana na kutowajibika huku nguvu zote zikiwa chini ya mtu mmoja.
 
Mf ishu ya Lissu mpaka leo, hatujui nini kinaendelea, wakati yule mbwa kapotea unakumbuka tamko lililotolewa?
Kwanini kwa binadamu isiwe hivyo ili at least tuone kuwa wanajali utu, japo changamoto ni nyingi?
 

Mkuu usisahau umasikini wa kipato tulionao ambao pia unatufanya masikini wa maarifa. Wenzetu walishamaliza suala kuziweka sawa taasisi zao za elimu hivyo pia suala la ulinzi na usalama wameliweka vizuri.
Ulofa tulionao unatunyima fursa ya kuwapa elimu ya uhakika ya masuala ya upelelezi vijana wetu, pamoja na kumiliki zana za kisasa kama ulivyozitaja. Bado tuna safari ndefu lakini namiini tutafika hata kwa miaka 20 au 30 ijayo
 
Mtu aliyetekwa kila sekunde ina thamani. Huwezi tu kwenda baharini kama habari ulizonazo zinasema amepelekwa Kibaha au kuna gari jeusi limeonekana linakwenda katika misitu ya Mabwepande. Siku ya kwanza huwa ni very chaotic ndiyo maana kama mna resources za kutosha inabidi kutanda kila kona - majini, nchi kavu na angani kwa mtindo wa kokoro...

Mengine yote nakubaliana nawe !!!
 
Mf ishu ya Lissu mpaka leo, hatujui nini kinaendelea, wakati yule mbwa kapotea unakumbuka tamko lililotolewa?
Kwanini kwa binadamu isiwe hivyo ili at least tuone kuwa wanajali utu, japo changamoto ni nyingi?

Nilifikiri tupo kwa MO. Kwa Lissu huko nina maoni tofauti kabisa (yenye mlengo wa kisiasa); na kila kitu ukikichanganya na siasa tu basi kinavurugika.
 

Umeongea mkuu, naunga mkono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…