Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siasa za Bongo....

Wasaudi wameua mwandishi wa habari katika ubalozi wao, wakamkata kata kama ng'ombe na kwenda kutupa nyama msituni. Uturuki wana ushahidi wa sauti mwandishi huyo akiteswa hadi kuuawa. Lakini watu wanasubiri uchunguzi na ripoti rasmi kuhusu tukio hilo ndiyo wajiaminishe kwa uhakika. Ndivyo inavyopaswa kuwa.

Shida yetu kubwa, wakati mwingine, ni kuingiza siasa katika kila jambo. Kila mwanasiasa anataka kiki. Haya mambo ya kutekwa ni magumu sana na yanahitaji umakini wa hali ya juu. Na kwa sisi wenye vyombo hafifu vya kipelelezi na kiutendaji hali ni mbaya zaidi. FBI mpaka leo kuna kesi za kutekwa watu mpaka leo zimewashinda...

Ukweli utajulikana tu [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…