Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ka davet ni katoto tena kakija kaanze na kuamkia[emoji23][emoji23][emoji23]ila ka hendisamu[emoji85][emoji85][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Uwiiiii ungeweka ushahidi nikaone daah katakua katamu kama lolpop[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aisee.
 
Sherehe za mazishi ya aliyekuwa mmiliki wa klabu ya Leicester City ya England, Vichai Srivaddhanaprabha zimeanza mjini Bankok, ambapo zinaendeshwa kwa taratibu za dini ya Budha.

Maandamano yanayoongozwa na askari yameanza huku Mfalme wa Thailand, akiwaongoza maelfu ya watu wanaohudhuria akiwemo mjane wa Vichai.
 
Kwa mujibu wa ratiba ni kuwa maandamano hayo makubwa yatafuatiwa na mazishi ambapo sherehe za maombolezo zitafanyika kwa siku saba kuanzia leo nyumbani kwake mjini Bangkok.

Bilionea huyo alifariki Dunia Jumamosi usiku kwa ajali ya helikopta pamoja na rubani wake Eric Swaffer 53 na mpenzi wake ambaye ni rubani msaidizi na fundi wa ndege, Izabela Roza Lechowicz,46, pamoja na Miss Universe Thailand pia Miss Photogenic 2005, Nursara Suknamai na Kaveporn Punpare ambao ni wajumbe wa bodi ya klabu.
 
Ajali hiyo ilitokea wakati bilionea huyo mwenye miaka 60 akitoka kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa King Power, kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya West Ham United uklioisha kwa sare ya bao 1-1.
 
N’GOLO Kante ni miongoni mwa wachezaji wafupi wanaotamba kwenye Ligi Kuu England kwa sasa. Kimo chake kina urefu wa sentimita 168. Kwa ulivyo mchezo wa soka, yeye anahesabika kama mbilikimo kutokana na uasili wa mchezo huo, unaotoa nafasi kubwa zaidi kwa watu wenye vimo virefu na wale wa saizi ya kati.
 
Kuwa mbilikimo kwa namna kubwa kuna kunyima fursa ya kuwa mwanasoka mahiri duniani. Supastaa Lionel Messi ni mfupi, akisimama ana kimo cha sentimita 170. Lakini, naye si mbilikimo.

Sasa huko Amerika Kusini kuna michuano ya soka ya kusaka ubingwa wa bara hilo itakayohusisha timu za mbilikimo tu. Kilichoelezwa staa wa Barcelona, Messi ameunga mkono uanzishwaji wa michuano inayohusu jamii hiyo ya watu wafupi zaidi duniani.
 
Michuano yenyewe itaitwa Dwarf Copa America yani Copa Amerika kwa wachezaji mbilikimo na uzinduzi wake utafanyika katika Jiji la Buenos Aires, Argentina.

Dhamira ya kuanzishwa kwa michuano hiyo ni kutaka kuondoa ubaguzi wa kijamii unaofanywa dhidi ya mbilikimo, wakionekana kama ni watu wa ajabu.
 
Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina kwa wachezaji mbilikimo, Diego Serpentini amesema Messi amesapoti kwa nguvu zote michuano hiyo itakayofanyika Buenos Aires.

Serpentini alisema: “Nimekutana na Leo Messi na amesema amesikia mambo mazuri kuhusu michuano hiyo. Hivyo, kama amesikia, ina maana michuano itakuwa imemvutia jambo kubwa zaidi.”
 
Chile, Colombia, Marekani, Canada, Argentina, Brazil, Paraguay, Peru na Bolivia ndizo nchi zitakazoshiriki michuano hiyo huku Morocco ikipewa mwaliko maalumu wa kwenda kushiriki mikikimikiki hiyo kwa kuanzia.

Timu moja itakuwa na wachezaji saba uwanjani na goli lao litakuwa na vipimo tofauti na magoli ya kwenye viwanja vingine, urefu wa goli utakuwa sentimeta 170 na upana ni sentimenta 200. Magoli yake yanayowekwa kwenye soka la kawaida la urefu wake ni sentimeta 244 na upana ni sentimeta 732.
 
Facundo Rojas, nahodha wa timu ya Argentina anaamini watu wenye matatizo ya umbilikimo wamekuwa wakinyanyaswa sana duniani kote, hivyo anaamini kwa kupitia michuano hiyo wataonyesha hata wao wana vipaji maridhawa kwenye mchezo wa soka.

Rojas alisema: “Tumekuwa tukinyanyaswa na kundi kubwa duniani. Tunataka kulibadili hilo, kuonyesha tuna uwezo wa kucheza soka, kufanyakazi na kujifunza.”
 
Staa wa Brazil, Oromar Miranda alisema ndoto zake zimetimia kwa kucheza kwenye michuano hiyo rasmi na kutakuwa na makundi pia ya kushangilia ili kufanya michuano yenyewe kuwa na mvuto wa hali ya juu na hili ni jambo muhimu sana kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…