Utafiti huo umeenda mbali zaidi na kubainisha kuwa watu wanaotumia korosho angalau mara nne kwa wiki, walionesha kuondokewa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (coronary disease) kwa asilimia 37! Na iwapo mtu atakula sana korosho, hatari ya kupatwa na magonjwa huendelea kupungua zaidi.
Dondoo moja ya ulaji korosho na kujiepusha na magonjwa ya moyo yote mawili (coronary na cardiovascular), inasema kuwa chukua kiganja kimoja cha korosho tafuna au kijiko kimoja cha chakula kilicho jaa ‘nut butter’, kula hivyo mara nne kwa wiki