Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Novemba, 2018 ameungana na Maaskofu, Mapadre, Watawa na Waumini wa Kanisa Katoliki, kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Askofu Evaristo Chengula. Askofu Chengula alifariki dunia tarehe 21 Novemba, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa Matibabu. #RIP ASKOFU CHENGULA