Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mdukuzi: halloo massai unasemaje
Massai: safi rafiki_

Mdukuzi:nikikuuliza swali unaakili ya kujibu?_
Massai:uliza acha maneno yako.

Mdukuzi:nitajie wanyama kumi wa porini
Massai:swala watatu na tembo saba πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ‘†πŸΏ

copy and paste
 
.JANA Jumatano alikuwa uwanjani Paris dhidi ya Liverpool akionyesha makali yake, lakini nje ya uwanja jina la Neymar limeendelea kuhusishwa kuondoka Ufaransa na habari mpya muhimu imeibuka juzi.
 
Imebainika Neymar ana makubaliano na klabu yake ya PSG kuondoka hapo kama kuna timu itafika dau la Euro 200 milioni ambalo walitumia kumnasa katika dirisha kubwa la mwaka jana kutoka Barcelona.
 
Klabu mbili za Hispania, Real Madri chini ya Rais wake, Florentino Perez pamoja na klabu yake ya zamani zote zinadaiwa kumsaka kwa nguvu staa huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye ameshindwa kuendana na maisha ya Ufaransa.
 
Klabu mbili za Hispania, Real Madri chini ya Rais wake, Florentino Perez pamoja na klabu yake ya zamani zote zinadaiwa kumsaka kwa nguvu staa huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye ameshindwa kuendana na maisha ya Ufaransa.
 
Mwakilishi wa Barcelona, Andrew Cury tayari amekutana na Baba yake Neymar, Neymar Jr jijini London wiki iliyopita kwa ajili ya kuzungumza uwezekano wa mwanae kurudi Barcelona na imedaiwa uhamisho huo pia unapigiwa debe na staa wa Barcelona, Lionel Messi.
 
Real Madrid wanamuona Neymar kama mchezaji mwafaka zaidi wa kuziba pengo la staa wao wa zamani, Cristiano Ronaldo aliyehamia Juventus katika dirisha kubwa lililopita la majira ya joto kwa dau la Pauni 88 milioni.
 
Mpaka sasa Madrid hawajafanikiwa kuziba pengo la Ronaldo na wamekuwa wakisuasua katika michuano mbalimbali wanayoshiriki msimu huu na ujio wa Neymar utamaanisha kwamba Madrid watakuwa wamesajili mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa tangu walipofanya hivyo katika uhamisho wa Gareth Bale katika dirisha kubwa la mwaka 2013.
 
Kwa upande wa Barcelona, endapo watafanikiwa kumpata Neymar wataweza kumruhusu staa wao wa kimataifa wa Ufaransa, Ousmane Dembele kuondoka baada ya kusuasua tangu alipowasili kuziba pengo la Neymar katika dirisha kubwa la majira ya joto mwaka 2017.
 
Neymar alikwenda Ufaransa kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia akikimbia kivuli cha Messi, lakini anaamini mpango huo umekwama baada ya kushindwa kutamba katika michuano ya Ulaya huku katika ligi ya ndani akionekana kukosa ushindani unaotakiwa.
 
Inadaiwa kwamba PSG pia wapo tayari kumuuza Neymar kwa sasa huku wakitaka kuunda timu yao kupitia kwa staa wa kimataifa wa Ufaransa, Kylian Mbappe, 19 ambaye nyota yake inaonekana kuifunika ile ya Neymar kwa sasa.
 
PSG pia wanaweza kulazimika kumuuza Neymar kutokana na kuhepuka matatizo na watu wa Uefa linapokuja suala la kanuni za matumizi ya fedha ambapo wameonekana kutumia pesa nyingi kuliko kipato chao tofauti na kanuni zinavyotaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…